Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen yuko
ziarani nchini Mali. Yuko mjini Gao kaskazini mashariki mwa nchi hiyo
ambako kuna kambi ya wanajeshi wa Ujerumani, wakiwa
katika ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa
Wakisaidia ulinzi wa amani katika makubaliano ya amani
yaliyofikiwa kati ya serikali na waasi. Vikosi vya Ujerumani
katika ujumbe huo vinatumia helikopta na ndege zisizo na rubani.
Jumatano wiki iliyopita hata hivyo helikopta moja ilianguka na
wanajeshi wawili waliuwawa katika ajali hiyo.Von der Leyen alikuwa amepanga ziara hiyo muda mrefu , lakini sasa yumo katika maombolezo. Waziri huyo jana Jumapili alishiriki katika sala ya kumbukumbu kwa ajili ya wanajeshi hao katika kambi ya Castor. Ripoti ya Jens Borchers kutoka mjini Gao inasomwa studioni na Sekione Kitojo.
Waziri Ursula von der Leyen akiwa katika sala ya kumbukumbu ya wanajeshi wawili waliouwawa mjini Gao
Katika
kambi ya Castor kumetengenezwa kanisa la muda. Kanisa la martin ,
hili sio kanisa halisi , badala yake ni hema tu lililopambwa kuwa
kanisa la muda. Katika kanisa hilo kumewekwa mishumaa pamoja na
picha za wanajeshi hao wawili waliofariki katika ajali hiyo ya
helikopta. Akiwa katika hali ya maombolezi Ursula von der Leyen aliimba na kusali pamoja na kiasi ya wanajeshi 100 hivi waliofika katika sala hiyo na baadaye aliwahutubia wanajeshi hao.
"Kupotelewa huku ni kugumu sana."
Tangu miaka miwili iliyopita hakuna mwanajeshi yoyote wa Ujerumani anayeshiriki katika ulinzi nje ya nchi ambaye ameuwawa. Katika eneo la Gao tumeshuhudia helikopta hiyo ikiwa imeanguka kilometa 70 kaskazini mwa mji huo. Pamoja na hayo ni lazima wanajeshi kuendelea na shughuli zao, kulinda eneo helikopta hiyo ilipoanguka na kupata taarifa zaidi.
Wasi wasi wa wanajeshi
Wanajeshi wengi wanaweza hapo baadaye kuwa na wasi wasi kuhusiana na kile kilichotokea. Ursula von der Leyen anataka kuzungumza nao na kuwasikiliza.
"Ndio sababu nataka leo kujumuika na wanajeshi na kutumia muda kuzungumza nao."
Ujumbe huo wa wanajeshi wa Ujerumani mjini Gao una wanajeshi 800. Amesema mchungaji anayehudumia jeshi hilo wakati wa sala jana kwamba , wiki hii ilikuwa ngumu sana kwetu.
Bado hijafahamika bado ajali hiyo ya helikopta ilisababishwa na nini. Kikundi cha wataalamu kimekwisha wasili na kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Waziri amezungumza na wataalamu hao, lakini matokeo kamili bado hayakuwekwa wazi. Moja kati ya visanduku viwili vya kunakili maelezo ya safari ya helikopta hiyo kimepatikana. Kimeharibika, lakini iwapo taarifa zitapatikana kutokana na kisanduku hicho, hilo halijafahamika.
Lakini leo hii mtazamo unaelekezwa katika mazungumzo na wanajeshi katika kikosi hicho mjini Gao. Von der Leyen hatapendelea kuzungumzia tu kuhusu kuanguka kwa helikopta hiyo. Anataka kuwapa motisha wanajeshi hao na kuzungumzia nao kuhusu ujumbe wao wa kulinda amani ulio ndani ya Umoja wa Mataifa.
Amesema von der Leyen kwamba yuko nchini Mali kuwapa moyo na kuwaunga mkono wanajeshi hao kwa kazi yao wanayoifanya, na kwamba mafanikio ya ujumbe huo ni hatua ya kuhakikisha usalama wa mataifa jirani. Na pia kuimarika kwa mataifa jirani ya Ulaya ni kuimarika pia kwa Ujerumani na pia Ulaya kwa jumla.
CHANZO: DW
SHARE
No comments:
Post a Comment