Katibu wa siasa na uenezi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, Dk.Zainab Gama ,akiwa na
Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Pwani, Mohammed Nyundo(MNEC)(picha na Mwamvua
Mwinyi)
…………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Zoezi la uchukuaji fomu kugombea
nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)2017,mkoani
Pwani,limeenda vizuri ambapo wanachama wamejitokeza kwa wingi kuwania
nafasi zilizotangazwa.
Zoezi hilo lilianza rasmi july 2
na kukamilika july 10 na sasa hatua inayosubiriwa itakuwa ni vikao vya
mapendekezo kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni.
Katibu wa CCM mkoani
Pwani,Anastazia Amas alisema, waliochukua fomu kugombea nafasi ya
wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa mkoani humo ni 11 na nafasi ya
mwenyekiti mkoa ni wanne.
“Wilaya ya Bagamoyo waliojitokea
kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti ni watatu,Kibaha Mjini ni
11,Kibaha Vijijini waliochukua fomu kwa nafasi hiyo ni watano”
alielezea.
Anastazia alisema waliochukua
fomu kuwania nafasi ya mwenyekiti wilaya ya Kibiti ni watano,Kisarawe
wanne,Mafia kumi,Mkuranga sita na Rufiji walichukua fomu hiyo wanne.
KATIKA HATUA NYINGINE, katibu wa CCM Kibaha Mjini,ABDALLAH
MDIMU Mdimu ,alibainisha,nafasi ya katibu mwenezi wamejitokeza watu
watano,wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya kwa makundi ya UVCCM,UWT na
Wazazi wamejitokeza watu 36.
Katika ngazi ya mkutano mkuu wa Taifa 30,mkutano mkuu wa mkoa ni watu 26 na halmashauri kuu ya CCM ya mkoa wamejitokeza watu 13.
Mdimu alieleza kwasasa hakukuwa na harufu ya kubebana wala kupanga safu kutokana na elimu waliyoitoa kuanzia ngazi za chini.
“Tulitoa elimu ya kutosha na kusimamia zoezi zima ,mabadiliko ya CCM Mpya kiukweli yameonyesha kila jambo linawezekana “
“Hakujitokeza hata mtu mmoja kuja
na mbwembwe kufuata fomu hata kurudisha na hakuna mtu ambae hajarudisha
fomu ,zoezi limefanyika kwa kufuata demokrasia na haki imetendeka kwani
wengi wamejitokeza ” alisema Mdimu .
WAKATI HUO HUO,mwenyekiti wa
jumuiya ya vijana (UVCCM)Mkoani Pwani ,MOHAMMED NYUNDO(MNEC) ,alisema
mchakato mzima upo vizuri na anaamini jumuiya hiyo wilaya na mkoa
itapata viongozi wenye uchungu na jumuiya/chama,waadilifu,wachap akazi na wawajibikaji.
Alisema wamekamilisha zoezi la
utoaji na urudishaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi mbali
mbali ngazi ya mkoa na wilaya .
Nyundo aliwashukuru vijana wote
kwa kuitikia wito katika zoezi hilo muhimu la mchakato wa kuwapata
viongozi wa jumuiya na chama kwa muda wa miaka mitano ijayo .
Alieleza wameridhishwa na idadi ya vijana waliojitokeza katika kuomba ridhaa katika nafasi zote.
“Ni wajibu wetu kuhakikisha
tunatenda haki katika nafasi zetu za kufanya mapendekezo.;Tunaahidi
kutenda haki,sisi tunaamini kila mmoja anayo haki ya kuomba, kuchagua na
kuchaguliwa.” aliongeza Nyundo.
Nyundo aliwasihi vijana wote,
kama walivyokuwa watulivu wakati wa kuchukua fomu, kujaza na kurejesha
bila aina yoyote ya matendo ya kuvunja kanuni za uchaguzi, basi wafanye
hivyo hivyo katika wakati huu wa kusubiri ratiba ya vikao vya maamuzi na
kuelekea kwenye uchaguzi .
Anasema kipimo cha kwanza cha kiongozi bora ni uvumilivu, na hasa katika kipindi hiki.
SHARE
No comments:
Post a Comment