TRA

TRA

Tuesday, August 29, 2017

Bulaya aruhusiwa kutoka Muhimbili, kupumzika siku 10

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja.

Bulaya alikimbizwa Muhimbili kutoka tarime mkoani Mara baada ya kupata tatizo la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya kituo cha polisi mjini Tarime. Alikuwa amelazwa wodi namba 18 katika jengo la Sewahaji akipatiwa matibabu.

Mbunge huyo wa Chadema aliruhusiwa Agosti 28 kutoka hospitali na amewashukuru madaktari wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu ya kina.

Amesema afya yake imetengemaa lakini amepewa maelekezo kadhaa.

“Kwanza nitapumzika kwa siku 10, hivyo ndivyo nilivyoagizwa na nitatakiwa kurudi tena hospitalini kwa ajili ya kuangaliwa afya yangu zaidi. Kwa sasa nitapumzika kabla ya kurudi jimboni kuendelea  na shughuli za maendeleo,” amesema Bulaya.


Bulaya aliwekwa rumande Agosti 18 baada ya kukamatwa na polisi akidaiwa kuingia jimbo la Tarime kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi kwa mwaliko wa mbunge mwenzake Esther Matiko.

Mwananchi:

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger