Baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii na picha zikisambaa
kutoka uwanja wa Taifa kwa madai kuwa, kipindi hiki ukarabati wa uwanja
huo sehemu ya pitch imeonekana fuvu la kichwa cha mtu, mkurugenzi
msaidizi wa idara ya michezo Alex Nkenyenge amevunja ukimya na
kufunguka yafuatayo;
“Kwanza hiyo ni taarifa ya uongo na hakuna fuvu isipokuwa ni madude
ambayo yamepatikana kwenye mchanga baada ya kuwa tumefukua sehemu ya
uwanja, kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa fuvu la mtu wala nini ni madude
tu yaani mamimea yale yaliyooza basi yanafanana kama magimbi ambapo
ndani lilikuwa limeshaliwa
“Sasa kwa sababu mtu analiona kwa mbali anasema fuvu sasa sijui fuvu
litakujaje hapa, kwanza kilichotokea hilo dude limekuja na mchanga wala
halikuwa ndani ya uwanja, yaani kwenye mchanga uliyoletwa ambao tulikuwa
tunajaza kwenye pitch baada ya kuwa tumeondoa lea ya juu
“Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho bahati mbaya kwa watanzania wanapenda
kuzungumza vitu vibaya kuliko vizuri, maana mtu haulizi wala kushangaa
ile inayosafisha uwanja, sasa kama ni fuvu unataka kusema uwanja wa
Taifa kulikuwa na makaburi?”
SHARE
No comments:
Post a Comment