OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeanzisha tena mchakato wa kupokea
maoni ya ziada kutoka kwa wadau vikiwemo vyama vya siasa kwa lengo la
kuboresha mfumo usajili na uratibu wa shughuli za vyama vya siasa.
Akizungumza na gazeti la Habarileo jana, Msajili Msaidizi wa Vyama vya
Siasa, Sisty Nyahoza ofisi yake imeuhisha mchakato huo tena baada ya ule
ulioanza mwaka 2013 kusitishwa kupisha mchakato wa utungwaji wa Katiba
na Uchaguzi Mkuu uliopita.
“Wazo la kutungwa sheria mpya ya vyama vya siasa ilitokana na maoni ya
wadau walioeleza kuwa sheria ya sasa ina mapungufu, na mwaka 2013,
tulipokea maoni kutoka kwa vyama vya siasa na asasi za kirai, sasa
tumewataka wadau kutuma maoni ya ziada kama wanayo,” alisema Nyahoza.
Alipoulizwa ni maeneo gani ambayo wamelengwa kuboresha, Nyahoza alisema
kwa sasa hawezi kubainisha maeneo hayo na kuwa wametoa fursa kwa wadau
kubainisha maeneo yenye upungufu.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewaandikia wadau vikiwamo vyama
vya siasa na asasi za kiraia ikiwataaka kupeleka maoni ya ziada baada ya
ofisi hiyo kupendekeza kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa
nchini.
Chanzo-Habarileo
SHARE
No comments:
Post a Comment