TRA

TRA

Tuesday, August 29, 2017

Israel: Iran inajenga kiwanda cha makombora Syria

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inajenga viwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeneza makombora.

Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kwa kuifanya Syria kuwa kambi yake kutengeneza vifaa vya kijeshi kama mpango wake wa kutaka kuiangamiza Israel.

Majeshi ya Iran yanamsaidia rais Bashar al Assad katika vita vya Syria huku ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Lebanon Hezbollah.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inatengeza kiwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.

Matamshi ya Netanyahu yanajiri baada ya kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutierrez mjini Jerusalem.
Bwana Guterres amefanya ziara yake ya kwanza katika enewo hilo tangu kuchukua mamlaka mnamo mwezi januari.
Bwana Netanyahu hakutoa maelezo kuhusu viwanda hivyo vya Iran lakini akaonya kwamba hicho ''ni kitendo ambacho Israel haitakubali''.
Wiki mbili zilizopita, kampuni ya Israel Imgesat ilichapisha picha ilizosema zinathibitisha ripoti ya gazeti moja la upinzani nchini Syria kwamba kiwanda cha makombora kilikuwa kikijengwa kaskazini magharibi mwa Syria chini ya uangalizi wa Iran.
Hakujakuwa na tamko lolote kutoka kwa Iran inayotaka taifa hilo Wayahudi kuangamizwa.
Bwana Netanyahu pia alimshinikiza Guterrez kuhusu walinda amani wa UN nchini Lebanon ,Unifil , ambapo Israel inadai wameshindwa kuwazuia wapiganaji wa Hezbollah kujiongezea silaha tangu vita vya 2006.
Bwana Guterres aliahidi kufanya kila awezalo ili kuhakikisha kuwa Unifil inaafikia malengo yake .
Ninaelewa wasiwasi wa kiusalama wa Israel na narejelea kwamba wazo hilo ama lengo la kuangamiza Israel ni swala ambalo halitakubalika kwa maoni yango.
Mkataba wa Unifil unatarajiwa kuongezwa mwisho wa mwezi.

CHANZO:BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger