Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa
benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro (kulia) akizungumza jambo na mmoja wa
wateja waliofika kwaajili ya kukabidhiwa magari makubwa ikiwa awamu ya
kwanza ya mkopo wa Magari Sita ambapo amepokea magari matatu na
matela matatu
Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa
benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akimkabidhi funguo
Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul
Dossa(kushoto) za magari matatu waliyokopeshwa na Benki ya NIC
Meneja Uendeshaji kutoka Kampuni ya
Usafirishaji ya Simera, Bw. Arif akiwasha moja ya gari mara baada ya
Benki ya NIC kukopesha magari sita kwenye kampuni ya Usafirishaji ya
Simera jijini Dar es Salaam.

Magari matatu kati ya sita yalikabidhiwa na benki ya NIC kama mkopo kwa mteja wao
Jana benki ya NIC imekabidhi magari
makubwa matatu na matela yake kati ya magari sita ambayo yamekabidhiwa
kama mkopo kwa Mteja wao Simera. Makabidhiano ya Magari hayo yamefanyika
katika Ofisi za FAW zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya
Simera, Bw.Zainul Dossa amepokea magari hayo kati ya sita
waliyokopeshwa na Benki ya NIC mapema jana huku magari mengine matatu
yatakabidhiwa hivi karibuni.
SHARE








No comments:
Post a Comment