Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Dkt. Paul Marealle
ameitisha kikao cha Kamati ya Tiba kitakachofanyika kesho Jumatano
Agosti 30, mwaka huu kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Kikao hicho kitakachofanyika
Ukumbi wa Ofisi za Makao Makuu TFF, yaliyoko Uwanja wa Kumbukumbu ya
Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kitarejea shughuli zake kwa
mujibu wa Katiba ya TFF sambamba na Kanuni zinazoongoza mashindano
mbalimbali ya TFF.
Katika kikao hicho, pia kamati
itapitia fomu za afya za utimamu wa mwili za wachezaji wote wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi
Daraja la Pili (SDL).
Miongoni mwa majukumu ya kamati
hiyo ni kupitisha wachezaji wanaopaswa kucheza/kushiriki katika ligi
baada ya kujirisha juu ya utimamu wa mwili wa wachezaji kwa michuano
tajwa hapo juu.
SHARE
No comments:
Post a Comment