Kampuni
ya Acacia, kwa ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme
kilichopo katika mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza
kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya mgodi huo.
Acacia
imewekeza shilingi bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha
maeneo yanayozunguka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine
ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga, Msalala, na sehemu nyingine za
Geita.
Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Haya
ni maendeleo makubwa kwa viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo
ambazo zitafaidika na uwepo wa umeme wa uhakika jambo litakalosaidia
kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji.
Mkuu
wa kitengo cha miradi ya maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu, Jiten
Divecha ameeleza kuwa tatizo la mabadiliko ya nguvu ya umeme limekuwepo
kwa muda mrefu na limekua likisababisha uharibifu mkubwa wa mashine.“Ujenzi
wa kituo hiki utasaidia kupunguza athari zinazotokana na kuongezeka au
kupungua kwa nguvu ya umeme katika migodi yetu hivyo kuboresha shughuli
za uzalishaji. Wakazi na viwanda vinavyotumia umeme katika wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga na wilaya zingine za mkoa wa Geita zitafaidika
na uwekezaji huu pia,” alisema Jiten.
Aliongeza:
"Acacia inajitahidi kuleta manufaa ya kiuchumi ya pamoja kwa jamii
zinazotuzunguka na wadau wake kupitia miradi endelevu."
Wakati wa ujenzi wa kituo hicho, ajira mbalimbali zilitolewa kwa jamii zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
SHARE
No comments:
Post a Comment