MAJAMBAZI sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha
Mamba wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana.
Miongoni mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa
wakielekea mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la
Madiwani Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana.
IGP SIMON SIRRO
Akizungumzia tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Chunya, Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo,
alisema tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la
Loge.
Shumbi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo
lililo na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga
barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na
wengine mapanga na fimbo.
Alisema watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya
basi wakiwaamuru abiria washuke, lakini iliwachukua abiria takribani
dakika 10 wakigoma kushuka kabla ya baadhi walioonekana kutishika zaidi
kuanza kushuka kwa kuruka kupitia madirishani.
Alisema baadaye iliwalazimu abiria wote kushuka na ndipo jambazi
wakaanza kuwasachi na kunyang’anya fedha taslimu na simu za mikononi
huku walioonekana kubisha, wakipigwa.
“Baada ya kushuka tulilazwa chini na kuanza kukaguliwa ambapo walichukua
fedha na simu na mimi mwenyewe ni mhathrika wa simu na fedha kidogo
nilizokuwa nazo. Ushauri wangu ni kuwa mabasi kama haya yaanze safari
saa moja asubuhi badala ya saa kumi na moja ama kumi na mbili,” alieleza
diwani huyo.
IMEANDIKWA NA JOACHIM NYAMBO- HABARILEO CHUNYA
SHARE
No comments:
Post a Comment