Mkutano
wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika SADC umemalizika tarehe 20 Agosti 2017 katika mji wa Pretoria
Afrika Kusini ambapo Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC kwa kauli moja
wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake katika Asasi ya Ushirikiano wa siasa , Ulinzi na
Usalama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kazi nzuri aliyoifanya
katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo.
Makamau
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi
na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa
mkutano huo mjini Pretoria.
Dkt. Stergomena Tax akila kiapo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .
Makamau
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi
na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa
mkutano huo mjini Pretoria. 
Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuteuliwa na kula kiapo kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .
(Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais )Tanzania imemaliza kipindi chake cha Uenyekiti
wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 19
Agosti, 2017 wakati wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
nchi wanachama wa SADC ambao umefanyikia hapa Pretoria, Afrika Kusini
kuanzia tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.Akizungumzia mambo muhimu
yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa 37 wa SADC, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye
amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amesema pamoja na mambo mengine SADC imetambua na kuthamini
mchango wa Tanzania katika kipindi cha Uongozi wa Asasi ya Saisa ,
Ulinzi na Usalama iliyokuwa chini ya Rais Dkt. John Pombe magufuli.
Amesema
Tanzania imeshakuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo mara tatu, kwa nyakati
tofauti ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni kipindi cha 2006/2007 na mara
ya pili ilikuwa ni 2012/2013 na mara ya tatu katika kipindi cha Agosti
2016 hadi Agosti 2017 chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo alikabidhiwa kijiti cha
uongozi huo kutoka kwa Jamhuri ya Msumbiji wakati wa Mkutano wa 36 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika Falme ya Swaziland tarehe 30
Agosti, 2016.
Miongoni
mwa mafanikio yaliyopatikana wakati wa Uenyekiti wa Tanzania katika
Asasi hiyo ni kusimamia uchaguzi wa Bungenchini Seychelles ambao
ulifanyika mwezi Septemba, 2016.
Aidha
katika kipindi cha Uongozi wa Tanzania ulisaidia kurejesha hali ya amani
na utulivu nchini Lesotho ambayo kwa muda mrefu tangu 2014 imekuwa
kwenye mgogoro wa kisiasa pamoja na kushughulikia matatizo ya Uchaguzi
nchini DR Congo.
Mkutano
wa 37 wa SADC pia umemuongezea muda mwingine Mtanzania Dkt. Stergomena
Taxi kuendelea na wadhifa aliokuwa nao wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa
kipindi cha miaka minne mingine ambapo atatumikia nafasi hiyo hadi mwaka
2021.
Dkt. Tax amethibitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliomaliza leo na kuapishwa rasmi kushika nafasi hiyo.
Mkutano
wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) umehitimishwa kwa kutolewa
Tamko (Communique) kuelezea yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na
Serikali ikiwa ni pamoja na mkutano wa 38 kufanyika nchini Namibia
Imetolewa na ;
Ofisi ya Makamu wa Rais
Pretoria, Afrika Kusini
20 Agosti, 2017.
SHARE








No comments:
Post a Comment