Marcos
Alonso amefunga mara mbili mabingwa watetezi Chelsea wakiifunga
Tottenham katika mchezo wao kwanza wa Premier League uliopigwa
Wembley.Vijana wa Mauricio Pochettino wanatumia uwanja Taifa kwa mechi
zao za nyumbani msimu huu kwa sababu uwanja wao wa White Hart Lane
unafanyiwa maboresho.
Mlinzi wa
pembeni Alonso alianza kuifungia Chelsea bao la kuongoza dakika ya 24
kabla ya Michy Batshuayi kujifunga wakati anaokoa mpira wa adhabu
uliopigwa na Christian Eriksen dakika 82 huku Alonso akiifungia bao la
ushindi dakika ya 87.
Msimamo wa EPL
V
SHARE
No comments:
Post a Comment