Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya
lililazimika kutumia risasi za moto kumdhibiti mtu mmoja ambaye alivamia
Bank ya NBC usiku akidaiwa kuingia baada ya kutoboa ukuta.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya Henry Mwaibambe amesema Jeshi
hilo linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu mtu huyo ambaye hakufahamika
jina wala umri ambaye alivamia Bank hiyo mara mbili.
”Jeshi la Polisi linaendelea kufanya
uchunguzi wa tukio la ajabu kidogo. Tarehe 19, Saa Sita na dakika Nne
usiku, mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake wala umri amefariki dunia
baada ya kujeruhiwa kwa risasi na askari Polisi waliokuwa kwenye lindo
la Bank ya NBC.” – Kamanda Mwaibambe.
SHARE








No comments:
Post a Comment