Utafiti
mpya uliofanywa Australia umeonesha kuwa wanawake wengi huvutiwa zaidi
na wanaume wenye tabia ya kula mboga za majani kwa wingi.
Timu ya Watafiti kutoka Macquarie University, Australia wamebaini katika
Utafiti wao kuwa wanaume ambao hutumia mboga za majani na matunda kwa
wingi huwa na rangi nzuri ya ngozi, hunukia vizuri na wanakuwa na afya
nzuri zaidi kuliko wanaume wanaokula vyakula vya wanga kwa wingi.
Watafiti hao pia wamebainisha kuwa wanaume ambao wanapenda kula nyama
kwa wingi miili yao hutengezeka harufu nzito ambayo haijabainishwa kuwa
ni nzuri au mbaya wakati wale wanaopenda kula vyakula vizito vya wanga
hutoa harufu isiyo nzuri.
SHARE








No comments:
Post a Comment