Muwezeshaji
kutoka PS3 Bw. John Machonchoryo
akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Semina kuhusu Mfumo Mpya wa
Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) jijini Mbeya. Katikati ni Katibu Tawala
Msaidizi, Mipango na Uratibu kutoka Mkoa
wa Njombe Bw. Amza Amen Ndossa na Muwezeshaji kutoka OR – TAMISEMI Bw. Jeremiah
Mtawa.
NA
FRANK SHIJA - MAELEZO
Katika
kuhakikisha inaongeza nguvu katika usimamizi wa Mifumo yote ya Sekta za Umma
iliyofanyiwa maboresho PS3 imejipanga kuwajengea uwezo watumiaji wa mifumo hiyo
katika eneo la usimamizi ili ifanyekazi kwa ufanisi na kuwa endelevu hata mara baada ya Program hiyo kumaliza muda
wake ifikapo 2020.
Hayo
yamebainishwa jana na Mkuu wa Timu ya Fedha kutoka Programu ya Uimarishaji wa
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dkt. Gemini Mtei alipokuwa akiongea na mwandishi
wa habari hizi wakati wa mafunzo kwa ajili ya watumiaji wa Mfumo mpya wa
Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) Jijini Mbeya.
Dkt.
Gemini amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya maboresho
katika mifumo mbalimbali iliyokuwa inatumika na Serikali na kuongeza kuwa jambo
kubwa la kutilia mkazo kwa sasa ni juu ya namna ambavyo mifumo hiyo itasimamiwa
ili iwe endelevu.
“Jambo
ambalo sasa tunatarajia kulitilia mkazo zaidi ni eneo la usimamizi wa mifumo ya
sekta za umma, tunataka kuona mifumo hii ikiendelea hata baada ya Programu yetu
ya PS3 itakapomaliza muda wake,” alisema Dkt. Gemini.
Alisema
kuwa kwa kutambua umuhimu wa usimamizi wa mifumo PS3 iliona haja ya kuendelea
na mifumo iliyokuwepo badala ya kuja na mifumo mipya jambo ambalo limewezesha
Serikali kuendelea kuwa msimamizi wa karibu wa mifumo hiyo.
Akizungumzia mafunzo hayo ya Mfumo mpya wa Uandaaji wa
Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep), Dkt. Gemini
amesema kuwa mfumo huo ni matokeo ya changamoto zilizoanishwa na watumiaji
(wafanyakazi wa serikali) ambao walibainisha maeneo ambayo wangependa yafanyiwe
maboresho.
Alizitaja
changamoto hizo kuwa ni pamoja na matumizi makubwa ya rasilimali fedha
itokanayo na mchakato mzima wa uandaaji wa bajeti uanzia ngazi ya kijiji ambapo
inahusisha rasilimali watu ambao wote wanahitaji kugharamiwa.
Dkt.
Gemini anesema kuwa baada ya kuainishwa kwa changamoto hizo TAMISEMI walikuja
na mapendekezo ya kuufanyia maboresho mfumo huo ambao umekuja kutatua
changamoto hizo ikiwemo kupunguza gharama kwa kurahisha mawasiliano kwa njia ya
Kielekroniki badala ya mtu kufunga safari kutoka sehemu moja hadi nyingine,
lakini pia kupitia mfumo huo mtumiaji ataweza kufanya marekebisho ya Bajeti
yake au taarifa yake bila ya kuchapisha nakala yote jambo linaloondoa gharama.
Kwa
upande wake Mtaalamu wa Masuala ya Tehama kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI James
Mtatifikolo amesema kuwa Serikali kupitia OR – TAMISEMI ndiyo yenye dhamana ya
kuisimamia mifumo hiyo baada ya kujengewa uwezo na PS3.
Mtatifikolo
aliongeza kuwa maboresho hayo ya mifumo hasa wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti
(PlanRep) ni kwamujibu wa mahitaji ya Sera ya Tehama na miongozo mbalimbali ya
Serikali.
Pamoja
na kuwa mradi wa huu PS3 unatekelezwa katika Mikoa 13 na Halmashauri 93 za
Tanzania Bara bado manufaa yake yanazifikia Halmashauri zote kupitia miradi
mbalimbali inayotekelezwa.
Katika
muendelezo wa kuwajengea uwezo watumiaji wa Mifumo iliyofanyiwa maboresho
Serikali kwa kushirikiana na USAID Tanzania/PS3 wanaendesha mafunzo ya nchi
nzima ambapo yanawashirikisha watumiaji wa mifumo ya PlanRep na Mfumo wa Fedha
(FFARS) ambapo washriki watano kutokoa Halmashauri 185 na wane kutoka mikoa
yote ya Tanzania Bara.
Muwezeshaji
wa masuala ya Tehama Bw. David Nyangaka akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Semina
kuhusu Mfumo Mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa
(PlanRep) leo Jijini Mbeya.
Muwezeshaji
wa masuala ya Tehama Jeremiah Mwambange akitoa
maelekezo kwa washiriki wa Semina kuhusu
Mfumo Mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya.
Baadhi
ya washiriki wa semina kuhusu Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti
katika Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia kwa makini mafunzo hay oleo
Jijini Mbeya. Mafunzo hayo yamelenga kuwa jengea uwezo watumiaji wa mfumo huo
katika Halmashauri zote nchini chini ya ufadhili wa USAD Tanzania/PS3(PICHA NA: IDARA YA HABARI – MAELEZO)
SHARE
No comments:
Post a Comment