Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto)
akizungumza wakati ugeni wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (kulia) ulipotembelea Banda la TADB katika
Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea
mjini humo.
NA MWANDISHI
WETU
WAZIRI wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameiasa Benki ya Maendeleo
ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwezesha wakulima ili waweze kuchangamkia fursa
za kuuza mazao ya kilimo nje ya nchi ili kuwaongezea kipato wakulima hao.
Waziri Hamad aliyasema hayo
alipolitembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa
Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
Mhe. Hamad alisema kuwa
Tanzania inapata fursa nyingi za masoko nje ya nchi kwa mazao mbalimbali
ikiwemo zao la karafuu, korosho na mazao ya mikunde ikiwemo dengu na mbaazi
zinazotakiwa sana nchini India na Arabuni.
“Naiomba Benki ya Kilimo
kuwawezesha wakulima wanaolima kibiashara ili kuchangamkia fursa za masoko kwa
mazao ya kimkakati yakiwemo zao la karafuu, korosho na mazao ya mikunde ikiwemo
dengu na mbaazi ambazo nchi nyingi marafiki wanahitaji,” alisema Mhe. Hamad.
Aliongeza kuwa wizara yake
inaletewa maombi mengi ya mazao kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nchi hizo.
Kwa mujibu wa Waziri Hamad
kuna wafanyabiashara wa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wanaohitaji zaidi ya
kontena mbili za korosho kwa wiki hivyo Benki ya Kilimo ina wajibu wa kuwezesha
wakulima ili waweze kuchangamkia fursa hizo.
“Naamini Benki ikiwawezesha
wakulima wanaweza kuchangamkia fursa za masoko ya nje ikiwemo ya
wafanyabiashara kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wanaohitaji zaidi ya kontena
mbili za korosho kwa wiki,” aliongeza.
Akizungumza wakati wa
akipokea ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa TADB ni kuchagiza juhudi za serikali za
kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania.
Aliongeza kuwa katika
kutekeleza hayo Benki ya kilimo imedhamiria na kujizatiti katika kuhakikisha
inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika
Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni
pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
“Lengo letu ni kuhakikisha
tuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha
kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na
kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.
Ameongeza kuwa Benki yake
imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta hizo ili kuongeza tija
sekta hizo ili kupambana na umaskini nchini.
Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akizungumza na viongozi wa
TADB alipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati
wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili
kulia) akiukaribisha ugeni wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (kushoto) ulipotembelea Banda la TADB
katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane
yanayoendelea mjini humo.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
ya TADB, Simon Migangala (kulia) akieleza machache kuhusu umuhimu wa Benki
ya Kilimo kwenye uchumi wa viwanda.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sarah V. Chiwamba akizungumza wakati wa Ziara hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga, (kushoto), akimkabidhi zawadi Mhe. Hamad.
Mhe. Hamad akitembelea
mabanda ya wakulima walionufaika na Mikopo ya TADB.
Mhe. Hamad akitembelea
mabanda ya wakulima walionufaika na Mikopo ya TADB.
SHARE
No comments:
Post a Comment