TRA

TRA

Monday, August 28, 2017

Tume ya Uchaguzi Yavitaka Vyombo vya Habari Nchini Kuiga Wenzao wa Kenya

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

1
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo wakati akizungumza na Mtangazaji wa AzamTv, Nurdin Selemani kupitia kipindi cha Mizani ya Wiki kilichorushwa jana Jumapili.
2
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani (kushoto)akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando baada ya kushirikia kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na Azam Tv Jumapili usiku.
3
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani (kushoto) ,akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na Taarifa ya TathminiBaada ya Uchaguzi huo.
Picha na Hussein Makame.
……………………….
Na Mwandishi Maalum
MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan amevitaka vyombo vya habari vya Tanzania viige mfano wa wenzao wa Kenya kwa kutumia muda mwingi kutoa elimu ya mpiga kura.
Akizungumza kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha AZAM Jumapili usiku, Ramadhan alisema moja ya mambo aliyojifunza katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya ni jinsivyombo vya habari vilivyoshiriki katika Uchaguzi huona kuchangia watu wengikujitokezakupigakura..
“Natamaninasisivyombo vya hapanyumbaniviigewenzao wa Kenya ambao walitoa muda mwingi kwa kutoa elimu ya mpiga kura,” alisema Ramadhani.
Bw. Ramadhani aliongeza kuwa baadhi ya mambo ambayo amejifunzakwa Tume Huru na Mipaka ya Kenya (IEBC) katika uchaguzimkuuuliomalizikahivikaribuni ni usambazaji wa vifaa katika vituo vya kupigia kura.
Alifafanua kuwa licha ya kuwa Kenya wana vituo vichachetakribani 40,000 vya kupigiakuraukilinganisha na vya Tanzania ambako kuna vituo 65,000, lakini alisema walifanya vizuri kwenye kusambaza vifaa.
Eneo lingine ambalo lilimvutia ni namna wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi katika Kituo cha kupigia kura wanavyokuwa na uelewa mkubwa kuhusu taratibu za kupiga kura.
Kuhusu kuruhusu wafungwa naWatanzania walioko nje kupigakura, Ramadhan alisema kwa sasa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi hairuhusu jambo hilo na akaongeza kuwa Tume haina pingamizi iwapo wabunge watatunga sheria inayoruhusu makundi hayo kujiandikisha na baadaye kupiga kura.
“Tume ya Uchaguzi hainamamlaka ya kuamuaninaniapigekura, ilatunaongozwa na katiba pamoja na sheria,” alisema.
Akizungumza utaratibu wa kupiga kura uliotumika Kenya,  Ramadhani alisema ni mzuri lakini akaongeza kuwa utaratibu unaotumiwa na NEC uko wazi ukilinganisha na  IEBC.
“Utaratibu wetu ni mzuri zaidi kwani unatoa fursa ya mawakala kujiridhisha kwamba mtu aliyeenda kupiga kura ndiye mwenyewe, unapunguzakelele,” alisema.
Akilinganisha teknolojia iliyotumiwa na IEBC, Ramadhan alisema inawezesha mtu akipiga kura inahesabiwa jambo ambalo ilisababisha  IEBC kutangaza matokeo ya awali ambayo hayajathibitishwa na akaongeza kuwa hilo ni jambo la hatari kwa kuwa matokeo ya pili yakibadilisha matokeo ya awali inaweza kuleta sintofahamu.
Alisisitizakwambamfumo ambao unatumiwana NEC badopia ni mzuri kwa kuwa unalengakutangazamatokeo ambayo yameshathibitishwa na yanaleta amani kwa jamii.
“Uchaguzi ulipitatulitangazamatokeo ya urais ndani ya saa 72 kwa hiyo tuliwahi kuliko wenzetu wa Kenya.”

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger