TRA

TRA

Monday, August 28, 2017

TUZO ZA AKINA KIBA NOVEMBA MWAKA HUU

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

ALI KIBA, NANDY WASANII PEKEE KUCHAGULIWA KWENYE TUZO ZA AFRIMA NOVEMBA 2017 KUTOKA COKE-STUDIO AFRIKA MSIMU HUU WAKIWAKILISHA TANZANIA. 

Ali Kiba na Nandy ndio wasanii pekee wa Tanzania wa Coke-Studio Afrika msimu huu ambao wameingia kuwania tuzo  za Afrima 2017, ambapo tuzo hizo zitafanyika Novemba mwaka huu.

Majina hayo yaliyotangazwa wiki hii jijini Lagos, yamejumuisha wasanii 18 kutoka Coke Studio Afrika watakao wania tuzo hizo za Afrimma 2017.

Ali Kiba na Nandy ndio wasanii pekee wa Tanzania wa Coke-Studio Afrika msimu huu ambao wameingia kuwania tuzo  za Afrima 2017, ambapo tuzo hizo zitafanyika Novemba mwaka huu.
Majina hayo yaliyotangazwa wiki hii jijini Lagos, yamejumuisha wasanii 18 kutoka Coke Studio Afrika watakao wania tuzo hizo za Afrimma 2017. Vipengele viliyotajwa ambapo wasanii hawa watawania ni Msanii Bora wa Kiume Afrika wa  mwaka, Msanii bora wa Kike wa Afrika wa mwaka, Kundi bora  la muziki Afrika, Rapa Bora wa Kiume Afrika, nyimbo bora ya kushirikiana, Wimbo Bora wa mwaka, Mwandishi Bora wa mwaka na Mtayarishaji Bora wa muziki.
Ali kiba ameweza kuchaguliwa katika vipengele viwili kuwania kuwa Msaniii Bora wa Kiume Afrika Mashariki akichuana na msanii kutoka Uganda, Eddy Kenzo. Pia Wimbo Bora wa kushirikiana “AJE” alioimba na M.I msanii kutoka Nigeria, akichuana na msanii kutoka Msumbiji  Jah Prayzah nyimbo “Watora Mari” aliooimba na Diamond Platinum na  Locko Ft. Mr Leo.
Wasanii wengine kati ya hao 18 ni Yemi Alade, AKA, Runtown, Nasty C, Eddy Kenzo, Locko, Anselmo Ralph, Jah Prayzah, Busiswa, Amanda Black, Kiff No Beat, Mafikizolo, Micasa, Bebe Cool, Nyashinski na Olamide wakishindania  vipengele tofauti.
Hii imekuwa ni mara ya nne kwa msaanii Ali kiba kuwania tuzo za Afrima, Pia imekuwa bahati ya kipekee kwa msanii wa kike Nandy kushiriki musimu huu wa Coke-Studio Afrika kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuwania tuzo za Afrima kwa mara ya kwanza.
Wasanii wa Tanzania wanaoshiriki msimu huu wa Coke-Studio 2017  ambao watafanya kolabo na wanamuziki kutoka nchini nyingine za Afrika ni Rayvany, Izzo Bizness, Ali Kiba  na Nandy. Baadhi ya wasanii wakali wengine kutoka Tanzania waliowahi kushiriki onyesho hilo ni Lady Jay Dee, Diamond Platinum, Vanessa Mdee, John Makini, Shaa, Ben Paul, Fid Q na kikundi  cha Zanzibar Culture Music Taarab.

Vipengele viliyotajwa ambapo wasanii hawa watawania ni Msanii Bora wa Kiume Afrika wa  mwaka, Msanii bora wa Kike wa Afrika wa mwaka, Kundi bora  la muziki Afrika, Rapa Bora wa Kiume Afrika, nyimbo bora ya kushirikiana, Wimbo Bora wa mwaka, Mwandishi Bora wa mwaka na Mtayarishaji Bora wa muziki.

Ali kiba ameweza kuchaguliwa katika vipengele viwili kuwania kuwa Msaniii Bora wa Kiume Afrika Mashariki akichuana na msanii kutoka Uganda, Eddy Kenzo. 

Pia Wimbo Bora wa kushirikiana “AJE” alioimba na M.I msanii kutoka Nigeria, akichuana na msanii kutoka Msumbiji  Jah Prayzah nyimbo “Watora Mari” aliooimba na Diamond Platinum na  Locko Ft. Mr Leo.

Wasanii wengine kati ya hao 18 ni Yemi Alade, AKA, Runtown, Nasty C, Eddy Kenzo, Locko, Anselmo Ralph, Jah Prayzah, Busiswa, Amanda Black, Kiff No Beat, Mafikizolo, Micasa, Bebe Cool, Nyashinski na Olamide wakishindania  vipengele tofauti.

Hii imekuwa ni mara ya nne kwa msaanii Ali kiba kuwania tuzo za Afrima, Pia imekuwa bahati ya kipekee kwa msanii wa kike Nandy kushiriki musimu huu wa Coke-Studio Afrika kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuwania tuzo za Afrima kwa mara ya kwanza. 

Wasanii wa Tanzania wanaoshiriki msimu huu wa Coke-Studio 2017  ambao watafanya kolabo na wanamuziki kutoka nchini nyingine za Afrika ni Rayvany, Izzo Bizness, Ali Kiba  na Nandy. 

Baadhi ya wasanii wakali wengine kutoka Tanzania waliowahi kushiriki onyesho hilo ni Lady Jay Dee, Diamond Platinum, Vanessa Mdee, John Makini, Shaa, Ben Paul, Fid Q na kikundi  cha Zanzibar Culture Music Taarab.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger