
Dar es Salaam Tarehe 21
Agosti 2017…Kampuni ya Uber nchini Tanzania imetangaza zana mpya maarufu
kama “Kuchati Ndani ya Programu” inayowawezesha madereva na wasafiri
kuandikiana ujumbe kwa kutumia programu hiyo bila malipo.
Kinyume na hapo awali
ambapo madereva na wasafiri wangetumia Ujumbe Mfupi (SMS) au kupiga
simu, zana hii inaleta unafuu kwa madereva na wasafiri hivyo basi
kuwapunguzia kadhia ya gharama za kupiga simu sambamba na kuharakisha
mawasiliano bila kuondoka kwenye programu ya Uber.
Maboresho haya ni juhudi endelevu za Uber na yanalenga kuimarisha wigo wa wasafiri na madereva wanapotumia programu ya Uber.
Zana hii mpya ni rahisi
sana kuitumia. Msafiri anapoita gari, kuna kitufe cha ‘Kuwasiliana’
kwenye menyu inayoonekana chini ya skrini. Wasafiri wanaweza kuwaandikia
ujumbe madereva, na madereva vivyo hivyo. Ujumbe utaonesha kwamba
umepokelewa baada ya kuutuma.
Kwa upande mwingine,
madereva watakiri kwamba wamesoma ujumbe kwa kugusa kwenye programu ya
Uber ili watume ujumbe wa ‘bomba’. Ili wasijichanganye barabarani. Aidha
wasafiri na madereva wanaweza kuona kama ujumbe wao waliotuma umesomwa.
Meneja Msimamizi wa Uber
nchini Tanzania Bw. Alfred Msemo amehoji kwamba, “Kila safari nzuri
huanza pale msafiri anapochukuliwa kwa gari, kwa hiyo tunajituma
kutafuta mbinu za kumchukua msafiri bila usumbufu wowote kwa msafiri au
dereva. Kipengele hiki cha Kuchati kitakuwa afueni kwa wasafiri na
madereva wanapotaka kuwasiliana ili kusaidiana kutafuta mwafaka wa
changamoto za safari kama vile, kufungwa kwa barabara au kutoa maelezo
ya mahali walipo.”
Kadhalika, kipengele
hiki kinatoa njia mbadala ya wasafiri na madereva kupiga simu wanapotaka
kuwasiliana. Hata hivyo, ili mtu atumie kipengele hiki anatakiwa awe
anatumia toleo la sasa la program ya Uber.
“Huu ni mwanzo tu wa
mchakato wa kuimarisha huduma za kutuma ujumbe moja kwa moja kwenye
programu ili kufanikisha wigo wa mawasiliano yasiyo na changamoto kwa
wateja wetu, na kuwasaidia kuwasiliana katika ulimwengu wa utandawazi na
ulimwengu halisi” amenukuliwa Bw. Msemo.
SHARE








No comments:
Post a Comment