TRA

TRA

Monday, August 21, 2017

Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa baada ya manowari ya jeshi la Marekani kugongana na meli ya kubeba mafuta pwani mwa Singapore, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani.

Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia.

Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa wanajeshi inaendelea.
Ndicho kisa cha pili kikubwa kinachoikumba meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni.


 Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore
Ripoti zinasema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu upande wake mmoja, lakini jeshi la Marekani lilsema kwa inaelea peke yake kwenda bandari ya Singapore.
Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singapore pamoja na walinzi wa pwani, wanafanya shughuli za uokoaji. Malaysia nayo imejiunga katika shughuli hiyo.
Kura taarifa kidogo kuhusu hali ya meli ya mafuta ya Alnic MC na wahudumu wake.
Meli hiyo ya mafuta inaripotiwa kuwa na uzito mara tatu wa manowari ya jeshi ya USS John McCain, na taarifa zinasema kuwa haikuwa imebeba mafuta wakati ya ajali hiyo.
Seneta John McCain ambaye jina lake limepewa manowari hiyo, aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa yeye na mke wake wanawaombea mabaharia hao.
Mwezi Juni mabaharia saba wa Marekani waliuawa wakati manowari ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya mizigo kwenye bahari ya Japan karibu na bandari ya Yokosuka.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger