Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kuelekea
Ndanda Day kesho, Timu ya Soka ya Ndanda inatarajia kushuka dimbani
kuumana na Kikosi cha Azam katika kuadhimisha siku hiyo kwenye Uwanja wa
Chamazi, Jijini Dar es salaam.
Mchezo
huo utakaoanza sa 10 alasiri utatanguliwa na burudani mbalimbali
ikiwemo muziki kutoka kwa wasanii wa bongo flava wenye asili ya Mkoani
Mtwara.
Akizungumza
kuelekea maadhimisho ya siku hiyo, Afisa habari wa Ndanda Idrisa
Bandari amesema kuwa katika siku ya kesho wataanza asubuhi kwa kwenda
kutoa huduma za kijamii hospitali ya Temeke wodi ya wazazi na kisha
kufuatiwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa bongo Flava.
Bandari
amesema, wasanii hao Wenye asili ya mkoani Mtwara Jay Mo, Amini, TID,
Msaga Sumu na Juma Nature anayetokea Mkoa wa Pwani ambapo watatanguliza
shughuli hiyo inayofanyika kwa mara ya nne ambapo mwaka huu itakuwa Mkoa
wa Dar es salaam ikiwa ni mara ya kwanza.
Kwa
upande wa Mshauri Masoko wa Ndanda, Peter Simon amesema kuwa kwa mwaka
huu Ndanda Day itafanyika mara mbili kwani wameamua kuifanya na Dar es
salaam kwani wanaamini kuna mashabiki wengi sana ndani ya Mkoa huu pia
ili kuwapa fursa mashabiki wao kuiona Ndanda mpya iliyo chini ya Kocha
Ramadhan Nsanzalwino mwenye asilia ya Burundi.
Meneja
Mkuu wa Masoko wa Mitsun Group ambao ni wadhamini wa Ndanda, Erhad
Mlyansi amewaahidi uongozi wa Ndanda kuwapatia bidhaa kutoka kampuni yao
ya Sayona kwa ajili ya kuwapelea wagonjwa siku ya kesho.
Nao
Wasanii wamewataka mashabiki wa Ndanda kujitokeza kwa wingi siku ya
kesho kwa ajili ya kuishuhudia timu yaon na kwa mwaka huu wanaamini
kutokana na udhamini walioupata basi timu yao ya Mkoani Mtwara itafanya
vizuri huku wakiahidi kutoa burudani ya kutosha.
Afisa
habari wa Ndanda, Idrisa Bandari akizungumza na wanahabari kuelekea
Ndanda Day itakayoadhimishwa kesho katika Uwanja wa Chamazi wakicheza na
timu ya Azam Fc ikiwa ni mara ya nne kufanyika kwa Tamasha hilo na
likisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Flava wenye Asili
ya Mkoani Mtwara pamoja na kutoa huduma za kijamii katika Wodi ya
wazazi Hospital ya Temeke. Kushoto ni mshauri wa Masoko wa Ndanda Peter
Simon akifuatiwa na wasanii wa Bongo Flava Jay Mo, Richie One na Amini.
Meneja
Mkuu wa Masoko wa Mitsuni Group,Erhard Mlyansi amewaahidi Ndanda
kuwapatia bidhaa zinazopatikana kutoka kampuni ya Sayona kwa ajili ya
kuwapelekea wakinamama kwenye Wodi ya wazazi Temeke Hospital siku ya
Kesho
Msanii
wa Muziki wa Kizazi kipya Khaleed maarufu kama Top In Dar 'TID'
akihamasisha mashabiki wa wana Mtwara kujitokeza kwa wingi siku ya kesho
Kuadhimisha Ndanda Day akiwa sambamba na wasanii wenzake Jay Mo, Richie
One na Amini.
SHARE
No comments:
Post a Comment