Zaidi ya wataalamu
100 wa teknolojia ya roboti wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua
ili kuzuia kundwa wa roboti zinazoweza kuua.
Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha.
"Wakati zitaundwa, zitawezesha vita kupiganwa kwa kiwango kingine cha juu na kwa haraka zaidi kuliko vile binadamu hufanya." barua hiyo ilisema.
"Hizi zitakuwa silaha za ugaidi, silaha ambazo magaidi watatumia dhidi wa watu wasio na hatia, na silaha ambazo zitadukuliwa kuhudumu kwa njia ambayo sio nzuri." iliongeza.
- Roboti yafanya upasuaji wa macho mara ya kwanza duniani
- Roboti inayohudumu kama polisi yazinduliwa Dubai
- Roboti 'mtoto' wa Toyota
- Roboti inayoweza kushiriki ngono kutengezwa
Kati ya wale walioweka sahihi barua ya mwaka 2015 ni mwanasayansi Stephen Hawking, na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple Steve Wozniak na bwana Musk.
Roboti za kuua ni zipi?
Roboti za kuua ni silaha ambazo zinaweza kuchagua na kuvamia kitu ambacho zinakilenga bila ya kuelekezwa na binadamu. Tayari kwa sasa zipo lakini kuboreshwa zaidi kwa teknolojia itachangia kuziwezesha kufanya hivyo.Wale wanaopendelea roboti hizo wanaamini kuwa sheria za sasa za vita zinatosha kutatua shida yoyote ambayo itaibuka ikiwa zitatumiwa.
Lakini wale wanaozipinga wanasema kwa roboti hizo ni tisho kwa binadamu na teknolojia yoyote ya kuziwezesha kuuwa inastahili kupigwa marufuku.
SHARE








No comments:
Post a Comment