
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani, Alhaj Majid Mwanga ,aliyesimama mwenye koti jeusi akizungumza
jambo na wananchi wa kijiji cha Kinzagu huko Lugoba,anaemfuatia kushoto
ni mwenyekiti wa kijiji cha Kinzagu William Meleck na diwani wa kata ya
Lugoba Rehema Mwene mwenye kilemba .(picha na Mwamvua Mwinyi )

Mwekezaji wa kampuni ya
Gulf.Conc.Khaled Mohammed ,akizungumza katika mkutano wa kijiji Kinzagu
kata ya Lugoba (picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MKUU
wa wilaya ya Bagamoyo,alhaj Majid Mwanga,amekemea tabia inayofanywa na
baadhi ya maafisa wa madini wasio waadilifu ambao wanakandamiza sheria
kwa maslahi ya matumbo yao na kuwanyima haki wananchi.
Aidha
amesema kuanzia sasa,afisa madini anayeingia kwenye vijiji vilivyopo
Chalinze na Bagamoyo, bila ya kupitia ofisi ya mkuu mkoa na wilaya hiyo
,mtendaji wa kijiji anapaswa amkamate na kufikishwa polisi.
Kutokana
na kemeo hilo,amemuagiza katibu tawala wa wilaya kuwaandikia barua
maafisa tarafa wote ,wapeleke taarifa za wawekezaji wenye leseni za
mifukoni na wasioendeleza maeneo yao.
Alhaj
Mwanga ,ameeleza pamoja na agizo hilo,serikali za vijiji zikae na
zipeleke taarifa za wawekezaji waliokwapua ardhi za watu bila
makubaliano na kupata ridhaa ya mkutano mkuu wa vijiji.
Aliyasema
hayo katika mkutano wa kijiji cha Kinzagu,huko Lugoba
/Chalinze,uliolenga kuzungumzia mgogoro baina ya mwekezaji Global co.ltd
,mwekezaji Gulf conc.na wananchi .
Alhaj Mwanga ,alisema atalala sambamba na maafisa madini wanaotengeneza migogoro kwa maslahi ya matumbo yao.
Mkuu
huyo wa wilaya ,alieleza ni lazima maafisa hao wafuate sheria na
kuheshimu mamlaka nyingine ,kwani kuna kila sababu ya kutambua ofisi ya
mkuu wa mkoa,wilaya,kata na vijiji.
Hata hivyo alhaj Mwanga alifafanua kwamba,wawekezaji wenye leseni zilizoegeshwa kimagumashi itakuwa imekula kwao.
Alieleza hatua hiyo itasaidia kuondoa wimbi la wawekezaji walio na leseni ambazo hazijafuata sheria .
Anasema,
kampuni ya Gulf ipo kwa mujibu wa sheria na wanaendelea na uzalishaji
wa madini ya kokoto ambapo kutokana na athari ya vumbi ndani ya jamii
alilazimika kuomba kuongeza eneo kwa ajili ya uzalishaji.
Anafafanua
,hatua mbalimbali zilifutwa kwa mujibu wa sheria ambapo kampuni hiyo
ilifanya tathmini kwa ushirikiano na maafisa ardhi wa halmashauri ya
chalinze .
“Baada
ya zoezi hilo kukamilika nilifika hapa na tayari nilisaini barua
niliyopaswa kusaini na kwasasa inasubiriwa mkuu wa mkoa
aipitishe,”alisema alhaj Mwanga .
“Cha
kushangaza baada ya uhakiki wa eneo linaloongezwa, inadaiwa alifika
kamishna msaidizi wa madini Kanda ya Mashariki kijijini hapa na kusema
eneo hilo ni la mwekezaji kampuni ya Global wenye leseni miaka 17
iliyopita “alisema .
Alhaj Mwanga alisema tamko hilo liliwachanganya wananchi na kampuni iliyokuwa na lengo la kulipa fidia wananchi .
“Afisa
huyo wa madini asingekuja kuzuia zoezi hili watu tusingefika leo hii
tena,kupoteza muda,gharama na kuacha mambo mengine ya
kimaendeleo:,”Maafisa hawa hata hawajui na hawajabadilika kwenda na kasi
ya Rais Magufuli ,bado wao wapo kwenye karne ya maslahi ya matumbo
yao”alisisitiza .
Alhaj
Mwanga aliwauliza watendaji wa chini wote na halmashauri juu ya taarifa
za mwekezaji Global na hakuna aliye na taarifa zake hata ofisi ya
wilaya hawaimtambui.
Nae mkazi wa Kinzagu,Mkombozi Mrisho alimuomba mkuu
wa wilaya kusimamia haki yao kwa kamishna wa madini mkuu ili waweze
kupata fidia na kuondoka katika eneo hilo ambalo ni hatarishi kwa afya
zao.“Mie nina umri zaidi ya miaka 17 aliyopewa leseni huyo Global lakini naapa hatumjui Global na hatujawahi kumuona tangu nizaliwe na kama kamishna huyo anamjua Global aseme alifanya tathmini mwaka gani “alisema Mrisho.
Mwakilishi
wa kamishna wa madini Kanda ya Mashariki, aliyefika katika mkutano huo
,afisa madini kanda ya Mashariki-Dar es salaam ,Antony
Ngalalumba,alisema kila mwekezaji lazima awe na leseni.
Alisema
,ni kweli wawekezaji wote wawili wanazo leseni, hivyo anabeba maagizo
ya mkuu wa wilaya na malalamiko ya wananchi ambapo atayafikisha kwa
kamishna mkuu wa madini ili kupatiwa ufumbuzi.
Akizungumzia
malalamiko ya maafisa madini kuingia vijijini bila kuonana na serikali
ya vijiji ,alieleza afisa yoyote akitaka kufika ndani ya jamii lazima
aione serikali ya kijiji kwa mujibu wa sheria ya madini 2010.
Ngalalumba ,alibainisha wawekezaji pia wanapaswa wawaone serikali ya kijiji badala ya kudharau serikali hizo kisheria .
Kwa
upande wake ,diwani wa kata ya Lugoba,Rehema Mwene,alitaka maafisa
madini kujenga ushirikiano na jamii na kuacha kukumbatia leseni za
magumashi kwa maslahi yao.
Alisema mwekezaji Global tangu apewe leseni hiyo mwaka 2001 hajawahi kuendeleza eneo lake na hakufuata utaratibu.
Rehema
,aliiomba serikali ya awamu ya tano kuchukua hatua kwa watumishi
wachache wanaokandamiza maslahi ya wananchi na kutumia raslimali za eneo
husika vibaya.
Mtendaji
wa kijiji cha Kinzagu Mauwa Mohammed.alisema kampuni ya Gulf ndio
wanaitambua ambayo inaendelea na uzalishaji na kukaa nao kwenye mkutano
wa kijiji kufanya makubaliano ya fidia.
Katika hatua nyingine,mwenyekiti wa kijiji cha Kinzagu ,William Meleck,alisema kitendo cha maafisa madini kuingilia zoezi la fidia ni kukwamisha maendeleo ya kijiji.
Alisema ,maafisa hao wanadharau serikali ya kijiji kwa kuingia kijijini pasipo ofisi ya kijiji kujua lolote huku wakidai taratibu zao sio lazima waripoti kwenye serikali za kijiji.
Mwekezaji wa kampuni ya Gulf.Conc.Khaled Mohammed ,alisema wakipata fursa hiyo wataendeleza ushirikiano wanaoufanya kijijini hapo.
Alisema kila siku wanazalisha awamu 50 za roli za kokoto na kuiingizia halmashauri ya Chalinze sh.milioni.tisa (9)kama ushuru kwa mwezi.
Katika hatua nyingine,mwenyekiti wa kijiji cha Kinzagu ,William Meleck,alisema kitendo cha maafisa madini kuingilia zoezi la fidia ni kukwamisha maendeleo ya kijiji.
Alisema ,maafisa hao wanadharau serikali ya kijiji kwa kuingia kijijini pasipo ofisi ya kijiji kujua lolote huku wakidai taratibu zao sio lazima waripoti kwenye serikali za kijiji.
Mwekezaji wa kampuni ya Gulf.Conc.Khaled Mohammed ,alisema wakipata fursa hiyo wataendeleza ushirikiano wanaoufanya kijijini hapo.
Alisema kila siku wanazalisha awamu 50 za roli za kokoto na kuiingizia halmashauri ya Chalinze sh.milioni.tisa (9)kama ushuru kwa mwezi.
Hata
hivyo Mohammed ,alieleza katika sekta ya afya tayari wamejenga nyumba
ya mganga ya kuishi familia mbili na sekta ya elimu wanasomesha watoto
wawili wa mazingira hatarishi elimu ya sekondari .
Kwa
mujibu wa Mohammed ,mwaka 2001 walipata leseni ya uchimbaji madini ya
kokoto Kinzagu kata ya Lugoba na wanatarajia kuongeza eneo kwa kulipa
fidia wananchi waliofanyiwa tathmini zaidi ya Milioni.650 .
Katika
mkutano huo ,uliadhimia kampuni ya Gulf.conc iendelee na shughuli zake
na kukamilisha zoezi la fidia huku likisubiriwa jibu kutoka kwa
kamishna mkuu wa madini.
SHARE
No comments:
Post a Comment