Mh. Selemani Jafo, alipokuwa
akifunga mafunzo ya siku tano kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa
Mikoa minane kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.
.Mh. Selemani Jafo, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tano
kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mikoa minane kwenye ukumbi wa
Hazina Mjini Dodoma huku Wakiwa wanamsikiliza kwa makini.
Mh. Josephine Matiro Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akitoa neon la Shukrani mara baada yakufungwa kwa mafunzo hayo.
Bibi Zainabu Chaula, Naibu
Katibu Mkuu Afya TAMISEMI, alipokuwa akitoa neon kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi kufunga Semina hiyo
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu
wa Wilaya wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufungaji wa Semina hiyo ya
siku tano. (Picha zote na Idara ya Habari Maelezo- Dodoma)
……………………………………………………………..
Na. Atley Kuni- TAMISEMI- Dodoma.
Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa
Mamlaka za serikali za Mitaa, kutoka katika mikoa minane hapa nchini
wame iahidi serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Mh. Dkt. John
Pombe Magufuli makubwa mara baara yakumalizika kwa mafunzo ya siku tano
yaliyo endeshwa na Taasisi ya Uongozi Institute kwa lengo
lakuwaimarisha watendaji hao wakuu katika ngazi ya Wilaya na Halmashauri
katika majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mjini, Josephine Matiro, amesema mafunzo
hayo yaliyo washirikisha jumla ya washiriki 84 kati ya 89 waliokuwa
wahudhurie yamewakumbusha majukumu yao lakini kuwaongezea uzoefu
kutokana na wao kutoka maeneo tofauti tofauti.
“Tulivyo kuja sio tunavyo ondoka,
miongoni mwetu tulikuwa tunagombana katika maeneo yetu sisi na
wakurugenzi lakini kupitia semina hii, tunaondoka tukiwa tumepatana”
alisema Matiko na kuongeza,
“Mhe. Naibu Waziri sisi tuahidi
kwamba, tunakwenda kubadilika kwani mafunzo haya yamekuwa na manufaa
makubwa, labda tuombe jambo moja mafunzo haya yawe ya mara kwa mara,
kwakuwa yanasaidia hata kupungua Pressure na stress za kukaa kituoni kwa
muda mrefu, tunapokutana hivi inatusaidia kubadilishana uzoefu.
Mh. Naibu waziri Selemani Jafo.
Akifunga mafunzo hayo, Naibu
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Mh. Selemani Jafo,
amewataka wakuu hao wa Wilaya na wakurugenzi, kuacha kuingiliana katika
utendaji badala yake wazingatie mipaka ya kazi inayo waongoza.
Mipaka ya kazi.
“Waheshimiwa wakuu wa Wilaya
ninyi mpo kwaajili yakumwakilisha Mh. Rais katika maeneo yenu, hivyo
msifanye Interference badala yake mkafanye intrevession, Wataalam na
mkurugenzi wakisha amua kama mkuu wa Wilaya vema mkashauriana kwa hoja
na kukubaliana kwa misingi yakujenga na sio kubomoa.”
Kero za Wananchi
Jafo amewataka Viongozi hao
kwenda kusimamia sheria, taratibu na kanuni bila ya kumuonea mtu, huku
akwasisitiza kwenda kujenga nidhamu na kutatua kero za wananchi ili kero
zinazo fikishwa ngazi ya Wizara zikomee huko huko kwakuwa katika ngazi
ya Wilaya na Halmashauri wapo wataalam wengi hivyo ametaka wataalam hao
watumike vema. “Matatizo yatakayo washinda basi vema mkayafikisha katika
Ngazi ya mkoa, sio kuwaacha wananchi wanalipa nauli zao kupeleka kero
Wizarani” Mh.Jafo
Vita ya Dawa zakulevya na Rushwa
Naibu waziri Jafo hakuacha
kuwahimiza viongozi hao kwenda kupambana na dawa za kulevya katika
maeneo yao, “Kapambaneni na vita dhidi ya dawa za kulevya, tunafahamu
dawa zakulevya imekuwa mwiba mchungu kwa nguvu kazi ya Taifa, tukailinde
nguvu kazi hii na agenda hii iwe ya kudumu katika vikao vyenu vyote vya
maamuzi”, “Aidha adui Rushwa msimuache akastawi katika maeneo yenu,
haiwezekani mgonjwa akakosa bomba la sindano.
Makusanyo kwa njia ya kieletroniki
Naibu Waziri Selemani Jafo
amewaagiza wakurugenzi kukusanya mapato kwa njia ya mifumo ya
kieletroniki na kuonya wale wote wanaofanya diversion ya mifumo
iliwarudi kwenye njia za kizamani, “Jiji la Dar es Salaam leo,
nimpongeze sana dada yangu Zipolla, amekuwa mfano wa kuigwa kutoka Mil.
15 hadi Mil 600 ya makusanyo ya ushuri wa maegesho ambapo hapo awali
wengine walishindwa hii ni hatua yakupigiwa mfano, ajenda ya mapato iwe
yetu sote.”
Usimamizi wa Rasilimali na thamani ya fedha.
“Lazima (value for Money) katika
miradi yetu yote mkaipe kipaumbele, jana nimetoa Press na maelekezo
yamekwenda tayari juu ya ukarabati wa Vituo 172 vya afya nchini kote
kwakuwa fedha hizo nimeelekeza mtumie force Account, niseme ule msemo
wa vijana wa mtaani, {Kipa katoka}, kazi kwenu lakini ifikapo Desemba
30, 2017 kazi hiyo iwe imekamilika alisema Jafo na kuongeza kuwa,
“Tulifanya vema katika shule kwenye zile Bil 25 leo watoto wote wapo
shule, tukafanye vizuri pia katika hili la Vituo vya afya”.
Mwisho Naibu Waziri Jafo hakuacha
kuwaonya Viongozi hao dhidi ya matumizi mabaya ya sheria inayowaruhusu
kuamuru kumuweka mtu rumande kwa saa 48, “sheria hii ipo lakini itumike
kunapo sababu sio kuitumia kiholela” alisema Mh. Jafo.
Salaam za Uongozi Institute
Akitoa salaama za Uongozi
institute Mkuu wa kitengo cha mafunzo Kadai Singo, alisema mambo
makubwa wanayotazamia mara baada ya mafunzo hayo ni pamoja na Weledi,
Mbadiliko, Wilaya zibadilike lakini kupata mrejesho wa matokeo chanya
baada ya mafunzo kukamilika.
Salaam za TAMISEMI na Dkt. Zainabu Chaula
Awali akitoa taarifa fupi juu ya
mwenendo wa mafunzo kabla yakumkaribisha Mh. Naibu Waziri kufunga
mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu Afya Dkt. Zainabu Chaula alisema, “Mara
baada yakukamilika kwa mafunzo hayo yaha shabaha ya Wizara ni kuwapatia
mafunzo ya aina hii Wah. Wakuu wa Mikoa ili katika utendaji wakawe na
uelewa wa pamoja”, Dkt. Chaula alimueleza Naibu Waziri aliyefika kufunga
mafunzo hayo.
Mikoa ambayo wakuu Wawilaya ambao
wamepatiwa mafunzo hayo katika awamu hii ilikuwa ni Shinyanga, Mbeya,
Rukwa, na Ruvuma, Mikoa mingine ni Songwe, Dar es Salaam, Njombe na
Iringa.
SHARE
No comments:
Post a Comment