
Kamanda wa polisi mkoani Pwani
(ACP)Jonathan Shanna ,wa katikati akizungumza na askari mbalimbali wa
mkoani hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi )
……………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
JESHI la polisi mkoani Pwani ,
limetoa onyo kwa askari wa vitengo mbalimbali mkoani hapo ,kuacha
kujihusisha na vitendo vya rushwa na atakabainika atachukulia hatua kali
za kijeshi.
Aidha jeshi hilo ,limejipanga
ipasavyo kwa kutumia askari waliopo katika kila himaya ili kupambana na
uhalifu kwa kuweka mikakati ambayo itakua ni muongozo na dira kwenye
utendaji kazi wake .
Akizungumzia suala la rushwa kwa
askari,kamanda wa polisi mkoa wa Pwani (ACP)Jonathan Shanna,aliwataka
wanaohusika na chumba cha mashitaka,upelelezi mdogo,kitengo cha
upelelezi na usalama barabarani wasiruhusu mianya hiyo .
Aliwaagiza kuhakikisha majalada
ya kesi yanafikishwa mahakamani na wapepelezi wa kesi hizo kuzisimamia
ipasavyo kwa kuwa jeshi la polisi ni chombo cha kisheria.
Kamanda Shanna ,alieleza hatakuwa
na muhali kwa watendaji watakaobainika kujihusisha na vitendo vya
kushawishi,kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa watuhumiwa ama
walalamikaji.
“Kuipa rushwa nafasi ni kuruhusu kushindwa kupatikana kwa haki kwa anaekusudiwa kuipata haki hiyo kisheria “
“Askari wawajibike ili kuondoa
mapungufu katika utendaji kazi ,wananchi wanategemea huduma iliyo bora
kutoka jeshi letu ,alisisitiza.
” Sitomvumilia askari
atakayekiuka maelekezo haya ,kila mmoja anatambua wajibu na mipaka yake
,sitategemea kupata malalamiko kutoka ndani ya jamii kufuatia utendaji
mbovu wa askari wangu “alisema kamanda Shanna.
Kamanda Shanna aliwaomba
wananchi watoe ushirikiano kwa viongozi wa jeshi la polisi na taasisi
husika ya kupambana na vitendo vya rushwa (TAKUKURU )ili kuwafichua
askari wote wanaofanya vitendo hivyo.
Hata
hivyo ,alieleza katika kipindi cha uongozi wake ameelekeza kuanzia kwa
maafisa ,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kufanyakazi kwa weledi na
usasa ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa wakati .
Kwa
mujibu wa kamanda Shanna ,anatambua mchango wa kila mmoja wao kwa
nafasi yake kwenye jitihada za kukomesha vitendo vya uhalifu .
Alisema
ana imani na utendaji kazi wa askari wote katika vikosi vyao ,uwezo wao
na uwajibikaji wa kila siku kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
uhalifu .
Kamanda
Shanna ,hakusita kutoa rai kwa wananchi kuzidi kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi kwa kuwafichua wahalifu waliopo kwenye maeneo yao ili
wachukuliwe hatua za kisheria .
Anasema kwa kufanya hivyo itawezesha kutokomeza uhalifu mkoani Pwani .
SHARE
No comments:
Post a Comment