TRA

TRA

Saturday, September 9, 2017

Gwiji wa muziki wa country afariki dunia

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa country kutoka Marekani Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Mzaliwa huyo wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, afisa anayesimamia mawasiliano yake ametangaza.

 Don Williams alianza kuimba muziki kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971
Williams alianza kuimba nyimbo kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971, na tangu wakati huo alichomoa nyimbo 17 zilizogonga chati za muziki wa country.

Nyimbo zake zilizovuma zaidi ni pamoja na Gypsy Woman na Tulsa Time, ambazo ziliimbwa tena na wanamuziki wengine kama vile Eric Clapton na Pete Townshend. Williams alitazamwa na wengi kama gwiji mnyenyekevu wa muziki wa country.

Nyimbo zake nyingine zilizovuma ni pamoja na You're My Best Friend, I Believe in You na Lord, I Hope This Day Is Good.
Mwanamuziki mwingine wa country kutoka Marekani Troy Gentry, pia amefariki, akiwa na miaka 50.

"Ni kwa huzuni kubwa ambapo tunathibitisha kwamba Troy Gentry, mmoja wa wanamuziki wawili wa country waliofahamika kama Montgomery Gentry amefariki katika akjali ya helikopta ambayo ilitokea mwendo wa saa saba mchana Medford, New Jersey," taarifa kwenye tovuti ya bendi hiyo ya wanamuziki wawili imesema.
Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.Wawili hao walikuwa wamepangiwa kutumbuiza Medford Ijumaa jioni.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger