Uzinduzi wa ligi soka ya
Defao CUP 2017 umefanyika katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa
kushirikisha jumla ya timu nane ambazo ni Minyinga, Makiungu, Mungaa,
Unyaghumpi, Siye, Kinku, Wibia pamoja na Unyang’ongo.
Katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo, timu ya Unyaghumpi ilikubali kipigo cha bao 2-0 kutoka timu ya Wibia.
Mwandaaji wa ligi hiyo, Salumu
Mtaturu maarufu kwa jina la Defao, alisema lengo lake ni kuhamasisha
vijana wilayani Ikungi hususani Kata shiriki za Makiungi, Mungaa na Puma
ili kutazama fursa zilizopo kwenye Kata zao na kuzitumia ipasavyo kwa
ajili ya matokeo chanya ya kimaendeleo.
“Lakini pia tumelenga kutafuta
kikosi kitakachojumuisha vijana kutoka Kata zinazoshiriki ligi hii ili
tuweze kuunda timu ya vijana itakayoweza kushiriki ligi mbalimbali
kuanzia ngazi ya wilaya ambapo tayari tumeanza taratibu za usajili wa
timu hiyo”. Alisema Defao.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo
uliofanyika Oktoba 25,2017 alikuwa diwani wa Viti Maluumu Zainabu Khamis
aliyeongozana na viongozi mbalimbali akiwemo diwani wa Kata ya Puma na
Wenyeviti wa Vijiji vya Makiungi, Wibia pamoja na Unyang’ongo.
“Niwaase vijana kutumia mashindano
haya kama chachu ya kujitoa kwenye makundi yasiyo na tija katika jamii
yakiwemo ya uvutaji bangi”. Alisema mgeni rasmi huku akimpongeza kijana
Defao (20) ambaye ni mhitimu wa chuo kwa kuanzisha ligi hiyo.
Wadau mbalimbali wa michezo
wanahimizwa kujitokeza kuongeza nguvu kwenye michuano hiyo hususani
kwenye suala la zawadi ambapo hadi sasa zawadi zilizopangwa ni mbuzi
pamoja na mpira mmoja kwa ajili ya mshindi wa kwanza, mshindi wa pili
mpira mmoja pamoja na Tsh.20,000 huku mshindi wa tatu akijishindia mpira
mmoja.



SHARE








No comments:
Post a Comment