
Askofu
Msaidizi jimbo la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini pamoja na Mhashamu
Eusebius Nzigilwa wa jimbo kuu katoliki la Dar es salaam wamefunguka na
kutoa taarifa kuwa wameamua kurudisha mgao wa fedha za Escrow ambazo
walipewa na James Rugemalira.
Viongozi
hao wa dini wamesema wameamua kurudisha fedha hizo za serikali kutokana
na kuwepo kwa kesi mahakamani ya kuhujumu uchumi inayomkabili James
Rugemalira ambaye ndiye aliwapa fedha hizo.
Mhashamu
Method Kilaini alidaiwa kupewa jumla ya fedha za kitanzania milioni
80.5 huku Eusebius Nzigilwa akidaiwa kupewa jumla ya milioni 40.4

SHARE
No comments:
Post a Comment