
Simbachawene
amefunguka na kusema kuwa amehushishwa kwenye sakata hilo kwa kuwa
alihudumu katika wizara hiyo na kusema lakini yeye hakuhusika kwa lengo
la kuhujumu uchumi wa taifa wala hakuwa na lengo baya kwa nchi.
"Kampuni
ambayo ilikuwa na ubia na serikali iliamua kumuuzia mtu mwingine ili
aje kufanya kazi na serikali kwa hiyo zilikuwa ni 'private arangement'
ambazo lazima wazilete serikalini sasa hata kama angebaki yule wa mwanzo
au huyu alichukua bila shaka matokeo ya kutokuwa na faida katika
uendeshaji wa rasilimali hii yangekuwa ni yale yale, kwa hiyo uhusika
wangu na kutajwa kwangu bila shaka ni kwa sababu nilihudumu kwenye
wizara ile lakini nina imani ya dhati ya moyo wangu kwamba uhusika wangu
haukulenga kuhujumu taifa, haukuwa wa maslahi binafsi bali ni katika
majukumu ya kiutendaji" alisema Simbachawene
Tangu
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo ya kuwataka wateule wake wote ambao
wamehushishwa kwenye ripoti hizo mbili za madini zilizoundwa na Spika
Job Ndugai kupisha ni mawaziri wawili wamethibitisha kufanya maamuzi
hayo akiwepo Simbachawene pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani.
SHARE
No comments:
Post a Comment