Manchester United imeanza
vyema michuano ya UEFA Klabu Bingwa Ulaya kwa kuizaba FC Basel kwa mabao
3-0. Mchezo huo wa kwanza wa kundi A ulichezwa kwenye uwanja wa Old
Trafford.
Mchezo mwingine wa Kundi A ulikuwa kati ya Benfica na CSKA Moscow, ambapo wageni waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.
Mabingwa wa England Chelsea nao walianza michuano hii kwa kutoa kisago cha nguvu baada ya kuichapa FC Qarabag kwa magoli 6-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, London. magoli ya Chelsea yalifungwa na Pedro (dk 5), Zappacosta (dk 30), Azpilicueta (dk 55), Bakayoko (dk 71), Batshuayi (dk 76 na 82).
Kwingineko Paris Saint- Germain iliizaba Celtic mabao matano kwa sifuri, Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani wakicheka na nyavu katika mchezo wa kundi B. Bayern Munich pia walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Anderlecht.
Barcelona pia ilianza vizuri kwa kuichapa Juventus kwa magoli 3-0, Messi akifunga mawili na Ivan Rakitic la tatu.
Sporting Lisbon wakicheza ugenini walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Olympiakos. Mcezo pekee uliomalizika bila magoli ulikuwa kati ya Roma dhidi ya Atletico Madrid.
SHARE
No comments:
Post a Comment