
Mfanyabiashara Yusuf Manji
ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana kuwa yeye bado ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu na kudai kuwa hatambui
kuvuliwa udiwani kama ilivyotangazwa na Mstahiki Meya wa Temeke,
Abdallah Chaulembo September 6, 2017.
Manji ametoa malalamiko hayo,
kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili na wenzake mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo katika kesi hiyo ambayo Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai upelelezi haujakamilika
na Manji kudai ameona habari kupitia gazetini kuwa amevuliwa udiwani.
Amedai kama ni kweli amevuliwa Udiwani hatambui, kwani ana miezi 2 yupo gerezani na serikali inatambua kwamba yeye ni Diwani.
“Vikao vya awali vya udiwani wa
Halmashauri ya Temeke nilikuwa nahudhuria kwa kuwa naheshimu Mahakama na
kwa uzito wa hii kesi sikutaka kupeleka hata maombi ya dhamana
Mahakamani.
“Mahakama imuagizie DPP na
aiambie Halmashauri ya Temeke kwamba wamenikamata na ndio sababu ya
kutohudhuria vikao. Kama wanataka nihudhurie DPP aombe remove order nitolewe gerezani ili niende kwenye vikao.”
Pia Manji amedai kuwa kama hilo
haliwezekani, basi wamuandikie barua itakayoonyesha agenda ya vikao
vyote na yeye atazijibu kwa njia ya barua pia.
“Ninachotambua mimi ni Diwani wa
Mbagala Kuu na kama nimevuliwa au sijavuliwa udiwani sitambui. Tayari
nimetumia fedha zangu mwenyewe zaidi ya Tsh. Milioni 70 sio za
Halmashauri kwa ajili maendeleo ya wananchi wake.”
Aidha, amedai kuwa hiyo kesi ni
nzito na DPP hapaswi kuangalia upande wake wa kesi tu, kwani yeye
amechaguliwa na wananchi na anawasaidia.
Awali kabla ya kuelezwa hayo,
Wakili wa utetezi Seni Malimi alidai kuwa wanatarajia kuwasilisha maombi
ambayo ni ya siri katika tarehe ijayo.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu
Huruma Shaidi akautaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanalifanyia kazi
suala hilo, ambapo kesi imeahirishwa hadi September 18, 2017.
SHARE








No comments:
Post a Comment