
Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi za
Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa
taasisi hizo wakimsikiliza Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano
(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mikataba ya utendaji
kazi kwa taasisi na Mashirika ya Umma mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald
Mashindano (kushoto) akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya
Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa taasisi hizo
(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mkataba wa utendaji
kazi kwa taasisi hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald
Mashindano (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) wakiweka saini
katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya
Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria
toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald
Mashindano (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) mkataba wa
utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw.
Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya Bi. Martha Charles.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald
Mashindano (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma
(UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) wakiweka saini katika mkataba wa
utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald
Mashindano (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma
(UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii
jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO
……………………..
Na.Bushiri Matenda-MAELEZO
Ofisi ya Msajili wa Hazina inasema
kuwa Taasisi na Mashirika ya Umma sasa rasmi kutekeleza mkakati wa
utendaji kazi ili kujiendesha na kutoa gawio kwa Serikali yenye lengo la
kuchochea maendeleo kwa taifa na kuendelea kuboresha huduma bora za
kijamii.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Msajili Mkuu wa Hazina Dkt.Oswad Mashindano wakati wa hafla ya
kutia saini mkataba wa utendaji kazi baina ya Msajili wa Hazina na
baadhi ya Wenyeviti wa bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika
ya Umma nchini.
“Ofisi ya Hazina inasimamia
Taasisi mbalimbali takribani 265, ni vyema Taasisi hizo kwa kushirikiana
kwa pamoja zikasimamiwa vizuri ili kutoa huduma endelevu na kuchangia
katika uwekezaji wenye tija kwa taifa”,alisema Dkt.Mashindano.
Aidha alisema kuwa mwaka 2014-2015
Ofisi ya msajili wa hazina walifunga mkataba naTaasisi na Mashirika ya
Umma 71 kati ya 265 ambapo mkataba huo ulilenga katika maeneo manne ya
kiutendaji ambayo ni usimamizi katika rasilimali fedha , watu, utawala
bora na huduma kwa wateja.
Dkt. Mashindano aliongeza kuwa
Katika tathmini ya mkataba uliopita kupitia nyaraka mbalimbali ,
uchambuzi umeonyesha kuwa zipo baadhi ya dosari katika utekelezaji wa
makubaliano ya awali ambazo alizitaja kuwa asilimia 25 ya mpango
mkakati waliojiwekea Taasisi na Mashirika hayaendani na bajeti
waliojiwekea.
Pili malengo yaliyobainishwa na
Taasisis hizo hayaendani na mpango kazi , maeneo ya ya usimamizi wa
rasilimali watu na utawala bado kuna changamoto, eneo la ukusanyaji
mapato katika baadhi ya Taasisi bado ni ndogo pamoja na eneo la Huduma
kwa wateja linahitaji kusimamiwa ipasavyo na kuwepo kwa baadhi ya
Taasisi na Mashirika ya Umma kujaza matokeo ya kazi ambazo hazipo kwenye
utekelezaji wa mapango kazi.
“Katika utiaji wa sahihi, mkataba
huu unaohusisha zaidi ya Taasisi na Mashirika 30 naamini tutazingatia
kutatua changamoto zilizopo na kuweka mpango wa maendeleo endelevu”,
alisisitiza Dkt. Mashindano.
Naye spika wa bunge mstaafu ambaye
pia ni mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa bima wa afya Bi. Anna Makinda
alitoa neno kwa niaba ya wenyeviti wa Bodi wa Taasisi na Mashirika ya
Umma alisema ni vizuri tukatatua changamoto zilizojitokeza katika
uendeshaji wa mashirika ya Umma ili yajiendeshe kwa tija na maslahi ya
Taifa.
“Watendaji wakuu wa Taasisi za
Umma na wenyeviti wa Bodi tunawajibishwa na makubaliano haya,
tunategemewa sana katika kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa
ujumla”, alisema Bi. Makinda.
Aliongeza kuwa Taasisi za vyuo
vikuu vilivyoingia makubaliano haya watawajibika katika kuwatayarisha
vijana katika kuliletea Taifa maendeleo.
Wenyeviti wa Bodi na watendaji
wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa
kuzingatia miongozo iliyopo taratibu na Sheria zilizopo kwa kushirikiana
na Ofisi ya Hazina ili kuleta tija kwa watumishi wengine katika Taasisi
za Umma.
Mbali na majukumu iliyonayo Ofisi
ya Msajili wa Hazina pia inasimamia katika masuala yote ya uwekezaji
nchini, mitaji, malipo mbalimbali ikiwemo mishahara kwa watumishi wa
Umma.
SHARE








No comments:
Post a Comment