
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
uzinduzi wa Tamasha la Jinsia linalofanyika kwenye viwanja vya TGNP
Mabibo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao Dkt. Vicensia Shule (kushoto) wakati
wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Jinsia lililoandaliwa na TGNP
Mtandao

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea tuzo ya Uongozi
kwa kuwa Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke na kutambua mchango wake
katika kusimamia na kuhamasisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake
kutoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao Dkt. Vicensia Shule
(kushoto) wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Jinsia
lililoandaliwa na TGNP Mtandao.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
……………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Tamasha la
14 la Jinsia lililoandaliwa na TGNP Mtandao
Makamu wa Rais amesema Serikali
imechukua hatua mbali mbali ili kumuwezesha mwananke kujikomboa
kiuchumi, ikiwa pamoja na kuanzisha Benki ya Wanawake Tanzania,
kuanzisha mifuko mbali mbali ya uwezeshaji ukiwemo mfuko wa Maendeleo ya
Wanawake pamoja na kuhamasisha uanzishwaji wa SACCOS na VICOBA na
vikundi vingine vya kiuchumi pia serikali iliagiza Asilimia 30 ya zabuni
za serikali zipewe wanawake, vile vile iliagiza halmashauri zote
kutenga asilimia 5 ya mapato kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya
wanawake.
Alisema “ Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini umuhimu wa uzingatiaji wa
masuala ya jinsia katika kuchangia na kuharakisha maendeleo ya nchi”.
Mhe. Samia alitoa wito kwa wadau
wa maendeleo kushirikiana katika kuhakikisha Tanzania kama nchi
tunafikia lengo namba 5 la ajenda ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya
mwaka 2063 ya Afrika ya kuhakikisha Mwanamke ana haki sawa na mwanaume
katika Nyanja zote za kijamii na haachwi nyuma kwenye maendeleo.
Makamu wa Rais alisisitiza ni
muhimu kwa Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuzingatia vipaumbele vya kijinsia
kwenye mipango yake ya bajeti.
Makamu wa Rais alisema ili kufikia
usawa wa kijinsia lazima mwanamke apewe mbinu za kumuezesha kiuchumi na
lazima alindwe na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili aweze kusimama
imara kwenye majukumu yake mbali mbali.
Makamu wa Rais alihimiza pia Wanawake kusaidiana na kuinuana ili kufikia malengo .
Mwisho Makamu wa Rais aliwapongeza
TGNP na Kamati ya Kitaifa ya kuweka kumbukumbu za wanawake kwa ajili ya
kuwatambua, kuwaenzi na kuweka kumbukumbu za michango ya wanawake
katika nyanza mbali mbali za maendeleo.
SHARE








No comments:
Post a Comment