AFYA ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo imezidi kuimarika baada ya kudaiwa kuwa anaendelea vizuri.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Neema Mwangomo wakati akizungumza na gazeti hili ambapo alisema hali yake kwa sasa inaendelea vizuri na kwamba imeimarika vyakutosha hivyo anaweza kuruhusiwa.
"Hali ya Mwadhama kwa sasa inaendelea vizuri, kutokana na matibabu anayopata chini ya uangalizi wa madaktari hivyo hakuna wasiwasi kabisa,"alisema.
Askofu Pengo amelazwa katika taasisi hiyo tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo viongozi mbalimbali akiwamo Rais, Dk.John Magufuli alifika kumtembelea na kumjulia hali.
SHARE
No comments:
Post a Comment