Mkurugenzi
wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara
ya Elimu, Salum Mnjagila, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu, Prof.
Eustella Bhalalusesa akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano
la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP). Kushoto ni
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues. (Picha zote na Zainul
Mzige wa Modewjiblog).
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari kuhusiana na kongamano hilo la siku mbili linalofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa NACTE jijini Dar es Salaam.
Na Rabi Hume wa Modewjiblog
Katika
kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua yenye ubora zaidi, Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limepanga
kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi
kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao
umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati
ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara.
Akizungumzia
mpango huo katika kongamano la siku mbili la kutambua vipaumbele
vinavyotakiwa katika kuandaa mpango huo wa elimu, kwa niaba ya Kamishna
wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu
iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila alisema
mpango huo unatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kwa
kuanzia mwaka 2017 – 2021 ili kuona ni jinsi gani utabadili elimu ya
Tanzania.
Alisema
kupitia kongamano hilo wanataraji kuchagua baadhi ya vipaumbele ambavyo
wataona vinaumuhimu zaidi kuanza navyo kwa miaka mitano ya kwanza kwa
mpango huo na baadae wataanza utekelezaji wa vipaumbele ambavyo vitakuwa
vimepewa kipaumbele na washiriki wa kongamano hilo.
“Tupo
hapa kufanya tathimini ya vipaumbele ambavyo vimeletwa mbele yetu ili
tufanyie uchambuzi na tuone ni vipaumbele vipi tutaviweka kwenye mpango
wa miaka mitano katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” alisema
Mnjagila.
Nae
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu,
Makuru Petro ambaye ameshiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania
kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO alisema katika kuchambua
elimu ya Tanzania wamegundua kuwa elimu imekuwa ikishuka na hilo
linatokana na kuongezeka kwa wanafunzi wanaosajiliwa kuanza shule huku
kukiwa hakuna maboresho ambayo yanafanyika ili kuboresha elimu hiyo.
Alisema
baada ya uchambuzi kufanyika wanafanya tathmini ili kupata matokeo
ambayo watajadili kwa pamoja kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka
mashirika ya kiserikali na yasiyo ya serikali ili kupitisha vipaumbele
ambavyo vitafanyiwa kazi kati ya vipaumbele ambavyo wao waliwasilisha
kwa washiriki hao.
“Elimu
ya Tanzania hali sio nzuri tumefanya uchambuzi hata mashuleni hakuna
hali nzuri mfano hata Geita tumekuta darasa moja linatumiwa na wanafunzi
80 hadi 100 na hilo ni tatizo na baada ya kuchambua changamoto na
kuzifanyia tathmini tunazileta hapa ili tuchague vipaumbele vya kuanza
kuvifanyia kazi,” alisema Petro.
Nalo
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
kupitia kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Zulmira
Rodrigues alisema lengo la kuweka mpango huo ni kuboresha elimu ya
Tanzania kwa kuifanya kuwa bora na iliyo na usawa kwa makundi yote ya
jamii kwa matokeo mazuri ya baadae.
Alisema
kuna mambo ambayo yanatakiwa kupewa vipaumbele ikiwepo ni pamoja na
ubora wa elimu, fursa za elimu kwa makundi yote katika jamii na kujenga
uwezo kwa watendaji ambao wanatoa hiyo elimu kama ni walimu basi wawe
wanapewa mafunzo kuendana na wakati uliopo ili kuwa na kitu kipya
ambacho kinahitajika kwa wanafunzi kwa wakati huo.
Mkuu
wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini
Ufaransa, Anton De Grauwe akiwasilisha vipengele mbalimbali
vinavyotakiwa kujadiliwa na washiriki wa kongamano hilo katika kuandaa
Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akiwasilisha mambo mbalimbali
muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye Ajenda 2030 ya elimu na mpango wa
utekelezaji katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta
ya Elimu (ESDP).
Ofisa
Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Jennifer Kotta (kushoto) akiteta jambo na Maofisa wenzake
kutoka UNESCO, Faith Shayo (katikati) na Leonard Kisenha (kulia) wakati
kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa
mwaka 2017 - 2021 likendelea.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Bw. Makuru
Petro ambaye akishiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa
kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO kwenye kongamano hilo.
Mshauri
wa Taasisi ya kimataifa ya mipango ya elimu (IIEP)/UNESCO, Barnaby
Rooke akielekeza vipaumbele kwenye bajeti ya sekta ya elimu ambayo
inahitaji maboresho makubwa ili kuleta mabadiliko kwenye sekta elimu
nchini.
Moja ya 'Papers' zilizowasilisha kwa washiriki.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akishiriki
kwenye kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu
(ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za NACTE jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Joseph Sekiku akitoa
maoni kuhusiana na udhaifu wa mipango ya sekta elimu nchini ambayo
haitekelezeki wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya
Sekta ya Elimu (ESDP).
Bi.
Helena Reutersward, kutoka Ubalozi wa Sweden kitengo cha Elimu akitoa
maoni wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya
Elimu (ESDP) nchini linaloendelea katika ukumbi wa mikutano NACTE jijini
Dar es Salaam.
Pichani
juu na chini ni wajumbe walioshiriki kongamano hilo kutoka taasisi
mbalimbali za serikali, Wizara ya Elimu, Taasisi za Elimu na Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
SHARE
No comments:
Post a Comment