Mtu wangu wa nguvu najua imekuwa kawaida
kwa kila staa kuweka style ya nywele katika muonekano tofauti tofauti,
hususani katika muonekano ambao sio wa kawaida, yaani haujazoeleka
machoni mwa watu. Hadi kufikia August 2014 hii ndio ilikuwa TOP 10 ya
style mbaya za nywele kwa mastaa wa soka.
10- Raheem Sterling alikuwa katika hii
list ila wakati huo akiwa katika klabu ya Liverpool ya Uingereza,
Sterling kwa sasa anaichezea klabu ya Man City.
9- David James ni golikipa wa zamani wa
timu ya taifa ya Uingereza na vilabu vya Liverpool na Manchester City,
style yake ya nywele iliingia kwenye headlines hizi.
8- Rene Higuita ni golikipa wa zamani wa
timu ya taifa ya Colombia, ukiachana na style yake ya nywele kuwahi
kuingia katika list ya style mbaya za nywele, anajulikana kwa style yake
“scorpion kick” ya uokoaji mipira langoni.
7- Namba saba haikuwa ikimilikiwa na
mchezaji mmoja, ila mabeki watatu ndio walipata nafasi ya kumiliki
namba ya count down hii, kutokana na style zao za nywele kufanana, David
Luiz, Carles Puyol na Fabricio Coloccini.
6- Marouane Fellaini style yake ya
nywele haitofautiani sana na style ya nywele ya David Luiz, Carles Puyol
na Fabricio Coloccini ila Fellaini kapewa namba sita. Fellaini anatajwa
kuwa huenda umahiri wake wa kupiga sana mipira ya vichwa wakati akiwa
Everton ulitokana na msaada wa nywele zake.
5- Ronaldo de Lima style yake ya nywele
iliingia kwenye headlines katika fainali ya michuano ya Kombe la Dunia
mwaka 2002. Sababu ya Ronaldo kunyoa hivyo ni kutokana na mtoto wake
kushindwa kuwatofautisha na Roberto Carlos wakati wanacheza mpira
akiwaangalia kwenye TV.
4- Giovanni Simeone huyu ni mtoto wa
kocha wa sasa wa Atletico Madrid Diego Simeone ambaye style yake ya
nywele haikuishia kutajwa kuwa ni style mbaya pekee, ila inawezekana
ikawa ni style mbaya kuwahi kutokea katika historia ya soka.
3- Djibril Cisse jamaa aliwahi kutamba
na timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Liverpool kati ya mwaka 2004
hadi mwaka 2007, Cisse amekuwa akijulikana kwa kupenda kubadili mitindo
ya nywele kichwani, kitu ambacho kilimfanya pia kuwa maarufu ukiachana
na uwezo wake uwanjani.
2- Chris Waddle kwa Uingereza hii
ilikuwa moja kati ya style za nywele zilizowahi kuwekwa nakutamba licha
ya kuwa zipo katika count down ya stori 10 mbaya, Waddle alikuwa kiweka
mtindo huo wa nywele wakati akiwa Tottenham Hotspurs.
1- Taribo West katika count down hii
huyu ndio staa pekee kutoka Afrika aliyeingia kwenye hii count down,
staa huyo wa kimataifa wa Nigeria ambaye alistaafu kucheza soka miaka
kadhaa nyuma, ndio alikuwa katika rekodi ya kuwa na style mbaya ya
nywele kuliko wote.
SHARE
No comments:
Post a Comment