Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Serikali
haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na
kufaidi pesa za walipa kodi hususani wa kipatao cha chini na wale
maskinini.
Hayo
yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa akiwahutubia
wananchi wa wilaya hiyo.
Dkt.
Kigwangalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote
nchini kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu
hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.
“Serikali
haitowavumilia watumishi wazembe, hivyo tutaendelea kuwafungia mageti
na kuwashughulikia wale wazembe, tunataka watumishi wa umma wafanye kazi
ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi, mtumishi akizembea tutamtumbua
majipu, akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na
kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu,” alisema Dkt.
Kigwangalla.
Aidha
alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe
kazi na kutekeleza ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.
“Hatutomuonea
mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya
ya mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi,” alisema naibu waziri.
Hata
hivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule
kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na
hakuna michango yoyote.
“natoa
wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi
wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za
kuendeshea shule hizo,” alieleza Dkt. Kigwangalla.
Dkt.
Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama
watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kina
kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment