Ajali
mbaya iliyohusisha Magari matatu likiwemo Daraladal ya abiria
linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto kwenda Ubungo, imetokea
mapema leo asubuhi katika barabara ya Mandela eneo la Tabara Matumbi,
Jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine
zaidi ya 16 kujeruhuwa vibaya sana na kukimbizwa hospitali ya Amana,
Ilala kwa Matibabu.
Inaelezwa
kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo
liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma,
hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugonga na
Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu
Mnadani.
Jitihada za kuyatoa magari hayo zinafanyika sasa. Kama unaweza kutoitumia barabara hiyo asubuhi hii ni vema kuepuka msongamano
Muonekano
wa Daladala hilo baada ya kugongana uso kwa uso la Lori lililokuwa
limepakia Ng'ombe, eneo la Tabata Matumbi, Jijini Dar es salaam leo.
Askari wa Usalama Barabarani na baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
Baadhi ya Ng'ombe walikuwemo kwenye Lori hilo, wakiwa wamewekwa kando baada ya kuokolewa.
Kichwa cha Lori hilo, kikiwa Chini baada ya Ajali.
SHARE
No comments:
Post a Comment