Klabu ya
Yanga Wanajangwani leo Machi 8.2016 wamefanikiwa kurejea kileleni mwa
ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara (VodaCom Premier Legue-VPL) kwa
kuiangushia kipigo cha mabao 5-0 Wana Kimanumanu African Sports, mchezo
uliomalizika dakika chache zilizopitakwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam.
Wafungaji wa Yanga ni pamoja na Kelvin Yondani bao moja, Ngoma (1) Tambwe (1) Matheo (1).
Mchezo
huo wa aina yake, Yanga ilijihakikishia ushindi mapema baada ya kupata
mabao kuanzia kipindi cha kwanza tu cha mchezo na hadi kufikia kipindi
cha pili walikwisha jifikishia mabao 5-0 dhidi ya wanakimanumanu hao.
Kwa
ushindi huo, Yanga inarejea tena kileleni mwa ligi huku kwa kufikisha
pointi 50 na kuwashusha watani zao Simba SC ambao walikuwa wanaongoza
ligi hapo awali ambao sasa wamerudi hadi nafasi ya pili kwa kubakia na
pointi zao 48 za awali, huku Azam wao wakibakia nafasi hiyo hiyo ya tatu
kwa kuwa na pointi 47.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment