Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion Bw. Alex Msama akimpokea Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya
Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka
ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini
Kahama leo na kuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa,
Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba na aliyewahi kuwa mbunge
wa jimbo hilo Ndugu James Lembeli.
Waimbaji mbalimbali wametumbuiza
katika tamasha hilo ambalo ndilo limehitimisha matamasha ya pasaka ya
mwaka huu yaliyofanyika katika mikoa ya Geita , Mwanza na Shinyanga
katika kanda ya ziwa, Waimbaji hao ni Upendo Nkone, Jennifer Mgendi,
Boniface Mwaiteje, Martha Baraka, Goodluck Gozbert , Jesca BM,
Christopher Mwahangila, Ephraim Sekereti na wengine wengi. (PICHA NA
JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-KAHAMA)
Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya
Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka
ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa Kushoto
ni Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw.
Alex Msama akisalimiana na Bw. James Lembeli wakati alipokuwa akipmokea
kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama leo.

Mwimbaji Tumsifu Rufutu akiimba
huku akiwa amevalia kama manabii wa zamani wakati alipotumbuiza katika
tamasha la Pasaka mjini Kahama leo.
Mwimbaji Jesca BM akifanya vitu vyake jukwaani.
Mshabiki wa muziki wa injili wa
mjini Kahama Grace Boyo na rafiki yake Sara Shija wakifuatilia burudani
ya muziki wa injili iliyokuwa ikiporomoshwa na waimbaji katika tamasha
hilo.
Mwimbaji Faustine Munishi
akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa na viongozi
wengine mara baada ya kuimba nyimbo zake mbili katika tamsha hilo.
Msabiki wa muziki wa injili wa
mjini Kahama Grace Boyo na rafiki yake Sara Shija wakifuatilia burudani
ya muziki wa injili iliyokuwa ikiporomoshwa na waimbaji katika tamasha
hilo.
Mashabiki mbalimbali wa muziki wa injili wakipiga picha za Selfie katika tamasha hilo.
Mwimbaji Martha Baraka na wacheza shoo wake wakifanya vitu vyao jukwaani.
Tamasha hilo pia limehudhuriwa na watu mbali mbali kama unavyoona katika picha hii.
Mwimbaji Ephraim Sekereti akiimba nyimbo za kusifu na kuabudu katika tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Msama Promotion akipiga picha ya pamoja na waimbaji wa kwaya ya Grorius ya Kahama mkoani Shinyanga.
Mwimbaji Boniface Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani huku mashabiki wakicheza kwa furaha.
Mashabiki wakicheza kwa furaha katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akicheza na wanakwaya wa Kwaya ya Grorius ya Kahama.
Mwimbaji Jeniffer Mgendi akiimba jukwaani.
Mwimbaji Goodluck Gozbert akipagawisha jukwaa katika tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya
Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka
ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa akisoma hotuba kwa niaba ya waziri Profesa Mbarawa katika
tamasha hilo kushoto ni Alex Msama wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa na Mbunge wa jimbo la Kahama Mh.
Jumanne Kishimba.
Mwimbaji Upendo Nkone akiwaimbisha mashabiki wake wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
Mwimbaji Boniface Mwaiteje na Faustine Munishi kutoka nchini Kenya wakifanya mambo makubwa jukwaani kama wanavyoonekana.
Mwimbaji Faustine Munishi
akionekana kufurahiswa na mashabiki wakati alipokuwa akiimba jukwaani
kwa kushirikiana na mwimbaji Boniface Mwaiteje.
SHARE
No comments:
Post a Comment