Monday, May 30, 2016
MISS TANZANIA USA AEESHA KAMARA ATEMBELEA, KUONGEA NA KUTOA MSAADA KENTON HIGH SCHOOL
Miss
Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton
High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni
hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara
anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo
Miss
Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira
siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es
Salaam.
Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja. (P.T)
MAHAKAMA KUU KUANZISHWA KATIKA MKOA WA MARA
Na Lydia Churi- Musoma
Mahakama
ya Tanzania inakusudia kuanzisha Mahakama Kuu katika mkoa wa Mara ambapo
ujenzi wa jengo la mahakama hiyo unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka
huu.
Akizungumza
leo mjini Musoma katika ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za kimahakama
katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande
Othman alisema mkoa wa Mara unayo haki ya kuwa na Mahakama Kuu kwa kuwa
nia ya Mahakama ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Alisema
mahakama hiyo itajengwa kwa haraka na itamalizika katika kipindi cha
mwaka moja kwa kuwa fedha kwa ajili ya ujenzi huo tayari imeshatengwa
ambapo nyingine imetokana na msaada waliopewa kutoka Benki ya Dunia.
Alisema
kuanzishwa kwa mahakama hiyo katika Mkoa wa Mara kutawapa fursa wananchi
wa Mara ya kupata huduma kwa karibu zaidi na pia itasaidia kupunguza
kesi zilizoko mahakamani kwa haraka.
Awali
akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake alipomtembelea, Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Magesa Mulongo alimwomba Jaji Mkuu kuanzisha Mahakama Kuu katika
mkoa wake kwa kuwa asilimia 55 ya kesi zote za mauaji katika Mahakama
kuu kanda ya Mwanza zinatoka katika mkoa wa Mara hivyo mkoa huo unayo
haki ya kuwa na Mahakama Kuu.
Pamoja na
mkoa huo kuwa na kesi nyingi za mauaji, Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa
wa Mara pia unakabiliwa na kesi nyingi zinazohusu masuala ya ardhi kwa
kuwa ni asilimia 38.3 tu ya eneo zima la mkoa huo ndiyo eneo linalotuwa
kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli za maendeleo
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Mkoa wa Mara una wakazi zaidi ya milioni 1.3.
Alisema
Mkoa wa Mara una eneo lenye kilometa za mraba 30,150 ambapo asilimia 36
ya eneo hilo ni maji wakati asilimia 25.7 ni eneo lenye mapori na
hifadhi za Taifa ikiwemo mbugaya wanyama ya Serengeti.
Aidha,
Mkuu huyo wa mkoa aliisifu Mahakama ya Tanzania kwa kufanya kazi yake
kwa weledi ya kuzimaliza kesi zilizohusu mapigano ya koo zilizokuwepo
katika siku za nyuma mkoani humo kwa kuwa zimesaidia maeneo ya mkoa huo
kuwa salama hivi sasa na hayaonyeshi dalili za kujirudia. Aliongeza kuwa
eneo la haki likitulia hata masuala ya utawala yakuwa rahisi.
Jaji mkuu
Leo amehitimisaha ziara yake katika kanda ya Mwanza yenye mikoa ya
Mara, Geita na Mwanza ambapo alikuwa akikagua shughuli mbalimbali za
kimahakama katika kanda hiyo.(P.T)
MAANDALIZI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA 2016/2017 YAANZA RASMI
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na
waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na
Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika jana jijini
Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti,
2016.
Mwenyekiti
wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatuma Mrisho
akielezea umuhimu wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania
wa mwaka 2016/2017 katika mkutano wa wadau wa utafiti huo uliofanyika
jana jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia
mwezi Agosti, 2016.
Mkurugenzi
Mkazi wa ICAP Tanzania Dkt. Fernando Morales akizungumza katika Mkutano
wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka
2016/2017 uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika
nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.(P.T)
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA ZIARANI MKOANI MANYARA
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Manyara, Luccas Ole Mukusu, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM
mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa
huo Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na baadhi ya
watumishi wa CCM mkoa wa Manyara, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa
huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo
Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika
Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati leo Mei
30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika
Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati leo Mei
30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa
mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa,
mjini Babati leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Afisa Tawala wa mkoa huo,
Eliakim Maswi.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa
mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa,
mjini Babati leo Mei 30, 2016.
wakiagana baada ya mazungumzo.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiagana na Afisa Tawala wa mkoa
wa Manyara Eliakim Maswi baada ya mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Joel
Bendera (Katikati), alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini
Babati leo Mei 30, 2016.
AKAGUA JENGO LA OFISI YA CCM LILILOUNGUA MWEZI MACHI MWAKA HUU
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) apata maelezo kutoka kwa
Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndegesu Ndekobali, alipokagua athari za
kuungua jengo la CCM mkoa huo, lililopo mjini Babati. Jengo hilo
liliungua Machi 7 mwaka huu.
Luhwavi akimaliza kukagua jengo hilo.
Baadhi
ya viongozi wa CCM wakimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu
Luhwavi kuzungumza nao leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara
mjini Babati
Luhwavi akiingia ukumbini.
Luhwavi akiwa tayari ukumbini.
Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara, Ndekobali akitoa neno la utangulizi.
Baadhi ya watunishi wa CCM kutoka wilaya za mkoa wa Manyara wakimsikiliza Luhwavi.
Masoud Mbengua kutoka Kitengo cha Usalama na Maadili, Makao Makuu ya CCM akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara akimkaribisha Luhwavi kuzungumza
MILLION 100 NA TUSKER FANYA KWELI UWINI YAZINDULIWA NDANI YA KANDA YA ZIWA
Kikundi
cha TYT kikitoa burudani wakati uzinduzi wa promosheni ya Million 100
na Tusker Fanya Kweli Uwini kanda ya ziwa uliofanyika jijini Mwanza
-Cross Park Bar Igoma.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Kanda ya Ziwa wakicheza
kufurahia uzinduzi wa Tusker Fanya Kweli Uwini jijini Mwanza.
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Kanda ya Ziwa Patrick Kisaka
akitoa maelezo ya promosheni hiyo kabla ya kuzindua rasmi wakati wa
hafla fupi ya uzinduzi wa promosheni ya Million 100 na tusker Fanya
Kweli Uwini, iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Mwanza.
Baada ya kutikisa jiji la Dar es Salaam
na manispaa ya Moshi leo Kampuni ya Bia ya Serengeti imeendelea kuwapa
raha wateja wake kwa kuzindua promosheni ya Milioni 100 na Tusker- Fanya
Kweli na Uwini Kanda ya ziwa ambapo Millioni 100 za Tusker Lager
kushindaniwa.
Uzinduzi
huo uliofanyika jijini Mwanza Katika Bar ya Cross Park iliyopo Igoma
wilayani Ilemela, ulipambwa na maonyesho ya barabarani ambapo msafara
ulianzia Kiwanda cha Serengeti Igoma na kuishia Cross Pack Bar huku
ukipokelewa na shamrashamra za aina mbalimbali.
Promosheni
hiyo itawapa fursa wateja kujishindia pesa taslimu Milioni 1 kwa
washindi kumi (10) kila wiki kwa muda wa wiki kumi na kufanya jumla ya
Milioni mia kushindaniwa na Zawadi za bia kibao. Promosheni hii
ilizinduliwa rasmi na itaendeshwa kwa muda wa wiki kumi. Uzinduzi huo
ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kampuni hiyo pamoja na wana habari.
Hii
si mara ya kwanza kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti kuendesha promosheni
kama hii kwani ni wengi wameshanufaika kupitia promosheni mbalimbali za
mfumo huu na hata kubadili maisha ya watumiaji wa bidhaa zake kwa kiasi
kikubwa. Kupitia bia ya Tusker Lager Kampuni hiyo inaendeleza kile
kilichokuwepo cha kurudisha fadhila na kutoa shukrani kwa watumiaji wa
bia ya Tusker Lager.
Wateja
wanaweza kujaribu mara nyingi kadiri wawezavyo. Ili kuwa mshindi wa
Tusker milionea, washiriki wataingizwa moja kwa moja kwenye droo
kutokana na vocha walizojaza mahali walipopatiwa huduma na wataweza
kujishindia pesa taslimu na droo hizo zitachezeshwa kila wiki.
Mtumiaji
anapofungua bia ya Tusker Lager (500ml) chini ya kizibo anaweza kupata
kizibo cha ‘Tusker Milionea’ hii itamuingiza katika droo ya kupata
Milioni moja, au anaweza kupata ‘Bia ya Bure’ – hii inampa mteja bia ya
Tusker papo hapo alipohudumiwa na ikiwa atapata ‘Jaribu tena’ utaendelea
kuburudika kistaarabu ili kuongeza nafasi yako kuibuka mshindi.
Promosheni hii itasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini ili
kuleta ufanisi zaidi.
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo jijini Mwanza Meneja Mauzo wa Kanda ya ziwa wa
Kampuni ya Bia ya Serengeti Patrick Kisaka, aliwashukuru wageni wote kwa
kuja kuwaunga mkono na kusema kuwa uzinduzi wa promosheni hiyo ni muendelezo wa kile kilichoanza wiki mbili zilizopita ikiwa ni kutoa shukrani kwa wateja wao kwa kusapoti bidhaa zao.
Alisema
“kuendesha promosheni hii ni kurudisha shukrani kwa wajeta wetu kwa
kutuunga mkono na kusapoti bidhaa zetu, ambapo tunampa mteja sehemu ya
faida tuliyopata Katika mauzo yetu hivyo kuwapa wateja wetu wigo mpana
wa kujiinua kimaisha. Kupitia bia yetu ya Tusker Lager tunampa fursa
mnywaji na mdau wa bia hii kufanya kweli hivyo watumiaji wa bia ya
Tusker wanaweza kujishindia shilingi Millioni moja kwa washindi kumi kwa
muda wa wiki kumi ambao tutawapata kutokana na droo tutakazochezesha
kila wiki.”
Naye
‘Commercial Planning & Activations Manager’ wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti Denis Tairo alisema “Kanda ya ziwa ni sehemu muhimu sana kwa
soko letu, wadau wa jiji hili la Mwanza mmekua mstari wa mbele na haikua
rahisi sisi kufika hapa leo bila ninyi wadau wetu basi nasi tunasema
burudika na bia ya Tusker ili upate nafasi ya kushiriki katika
promosheni hii, haijalishi upo wapi na unafanya nini lakini amini kuwa
kila wiki ni Millioni kumi zinatolewa kwa watumiaji kumi wa bia ya
Tusker.”
Wapenzi
na wadau wa Tusker wataweza kushuhudia droo za Promosheni ya Milioni
100 na Tusker zitakazofanyika kila wiki siku ya ijumaa na kurushwa moja
kwa moja katika runinga. Washindi
watakaopatikana watakabidhiwa pesa zao ambazo watazipokea kwa njia ya
mtandao kila ijumaa inayofuatia kwenye hafla maalum ya makabidhiano.
Milioni 100 na Tusker Fanya kweli na Uwini itadumu kwa muda wa wiki kumi
nchi nzima.
Subscribe to:
Posts (Atom)