
Rais Ali Bongo Ondimba katika mkutano na waandishi wa habari Septemba 1, 2016.
Rais wa
Gabon Ali Bongo amesema Alhamisi hii kuwa "demokrasia enaeleweka vibaya
kwa kuvamia na kushambulia jengo la Bunge. " Ujumbe wa Bw Bongo ulikua
ukielekezwa kwa upinzani unaopinga kuchaguliwa kwake tena.
"Uchaguzi
umetoa uamuzi wake. Ni nani aliyepoteza? Kundi dogo ambalo mpango wake
ilikuwa kuchukua madaraka ili kunufaika kupitia nchi ya Gabon na wala
sio kuitumika nchi ya Gabon,"amesema Ali Bongo wakati wa hotuba yake kwa
vyombo vya habari.
Pia Waziri wa Mambo ya Ndani ametangaza kwamba maelfu raia wamekamatwa tangu Jumatano usiku.
"Katika
mji wa Libreville pekee, watu kati ya 600 na 800 wamekamatwa, na 200
hadi 300 katika maeneo mengine ya nchi," amesema Waziri wa mambo ya
Ndani wa Gabon, Pachomius Moubelet-Boubeya.
Jumuiya
ya kimataifa imetoa wito wa kukomeshwa kwa vurugu na kuanza upya zoezi
la uhesabuji wa kura za uchaguzi wa tarehe 27 Agosti.RFI
SHARE








No comments:
Post a Comment