Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha mfuko wa kubebea mbolea ya
kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa
mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri
Mkuu na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya
kumuaomba radhi Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. Kushoto
ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba na wapili
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda
cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea
hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu
na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya kumuaomba radhi
Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
*Ataka waandike barua ya kuomba radhi kwa Rais
Magufuli
*Aagiza Waziri wa Biashara aje na timu yake
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha
kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye
lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.
Kutokana na
hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa
Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari
22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.
Ametoa agizo hilo
leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo
wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri
Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za
kitaifa.
“Nilikuja
kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko
vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi.
Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina
anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.
“Ni kwa nini
mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je
mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania
haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na
uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda
ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”
Akiwa ndani
ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa:
‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani
ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu
lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park,
Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri
wa TBS.
Baadhi ya
mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa
wateja.
Pia amesema
atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage
aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara
(FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.
“Kwa staili
hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku
wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite
pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,”
amesisitiza.
“Tukiruhusu
hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi
yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa
njia hii kweli?”
“Nataka
wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua
ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.
Akitoa
maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans
alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na
wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe
radhi.
Waziri Mkuu
kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya
Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari
Singland.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.
SHARE
No comments:
Post a Comment