Emmanuel Macron, mgombea wa "En Marche!"
katika uchaguzi wa urais, anaongea na waandishi wa habari baada ya
mkutano wake na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin, Machi
16, 2017
Emmanuel Macron amekutana na Angela Merkel Alhamisi hii Machi 16
katika Ofisi ya Kansela huyo wa Ujerumani kwa muda wa saa karibu moja.
Baada ya mkutano huo, alielezea furaha yake na kusema ameafikiana mambo
mengi na kiongozi huyo wa Ujerumani, ambaye amempokea kwa mara ya kwanza
mjini Berlin.
Emmanuel Macron ameondoka katika Ofisi
ya Kansela wa Ujerumani akitabasamu. Kisha akaenda kukutana waandishi
wengi wa wa habari wa Ufaransa na Ujerumani ambao walikuwa wakimsubiri.
Mgombea wa En Marche! amebaini kwamba mazungumzo na Angela Merkel
yamefika "wakati muhimu wa kampeni. "Wakati ambapo ana matumaini ya
kuibuka mshindi wakati ambapo François Fillon amepoteza uaminifu kwa
sababu ya mashitaka yanayomkabili.
Nchini Ujerumani, hatari ya chama cha
Front National imechukuliwa kwa umakini. Suala hili limejadiliwa wakati
wa mkutano kati ya Emmanuel Macron na Kansela. Mgombea urais amesema
kwamba Bi Merkel ameonyesha "nia yake ya kufanya kilio chini ya uwezo
wake ili nchini Ufaransa baadhi ya vyama visiwezi kupata ushindi."
Pamoja na François Fillon ambaye ana matatizo makubwa, chaguo la Macron
linaonekana kuwa litachukuliwa kwa umakini nchini Ujerumani kwa kumzuia
Le Pen.
Emmanuel Macron amesema kama atashinda
ataimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa na Ujerumani. Na ana imani
kwamba ataibuka mshindi wa uchaguzi ujao.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment