Umoja wa Ulaya umesema uko tayari kuzungumza na Uingereza kuhusu
mustakabali wa mpango wa biashara huru, kabla pande hizo mbili
hazijakubaliana masharti ya mwisho kuhusu Uingereza kujiondoa kwenye
umoja huo.
Hayo yamo katika rasimu ya muongozo wa mazungumzo ya Umoja wa
Ulaya uliotolewa leo.
Muongozo huo ni pamoja na kusisitiza kipindi cha
mpito ambacho kitafuata Uingereza kuondoka mwaka 2019 na kabla ya
makubaliano ya biashara huria hayajasainiwa.
Uingereza lazima ikubali
masharti ya Umoja wa Ulaya ikiwemo kuchangia katika bajeti na usimamizi
wa mahakama, ambayo baadhi yake ndiyo sababu kuu iliyowafanya Waingereza
wapige kura ya ndiyo kujiondoa kwenye umoja huo, mwezi Juni mwaka
uliopita.
Muongozo huo umesambazwa leo na Rais wa Baraza la Ulaya,
Donald Tusk, kwa nchi 27 za umoja huo. Huenda muongozo huo ukaangaliwa
upya mwezi ujao kabla ya kuidhinishwa katika mkutano wa kilele wa Aprili
29.
SHARE
No comments:
Post a Comment