Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema,
(CHADEMA), leo Machi 15, 2017 amemsindikiza mahakamani Miss Tanzania wa
zamani ambaye sasa ni mwanachama wa CHADEMA, Wema Sepetu, ambaye
anakabiliwa na kesi ya kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam, ambayo ndiyo inayosikiliza kesi hiyo, imeiahirisha hadi
Aprili 11, 2017. Kwa sasa wema yuko nje kwa dhamana. Pichani, Wema akiwa
na Godbles Lema, wakati akitoka mahakamni hapo leo baada ya kesi
kuahirishwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment