TRA

TRA

Wednesday, March 15, 2017

Hedifoni zalipuka mwanamke akisikiliza muziki kwenye ndege Australia

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Maafisa wa serikali nchini Australia wametahadharisha watu dhidi ya kutumia vifaa vinavyotumia betri wanaposafiri kwenye ndege.
Hii ni baada ya headphone (Hedifoni/kifaa cha kusikilizia sauti kwenye simu na mitambo mingine ya kompyuta) zilizokuwa zinatumiwa na abiria mmoja kulipuka.
Mwanamke huyo alikuwa amelala akiwa kwenye ndege iliyokuwa safarini kutoka Beijing hadi Melbourne pale alipozinduliwa na mlipuko mkubwa.
Alizitoa hedifoni hizo, ambazo hutumia betri, upesi kutoka kichwani na akagundua zilikuwa zinatoa cheche za moto.
Zilishika moto na kuanza kuyeyuka.
Mlipuko wa headphone hizo ulimwacha akiwa na masizi usoni pamoja na malengelenge yaliyotokana na moto kwenye vidole vyake.
Mwanamke huyo ambaye jina lake limebanwa, ameambia Shirika la Usalama katika Uchukuzi Australia (ATSB) kwamba alikuwa akilisikiliza muziki mlipuko huo ulipotokea.
"Nilijishika usoni mara moja jambo lililosababisha hedifoni zangu kujikunja kwenye shingo. Niliendelea kuchomwa nazo na ndipo nikazishika kwa nguvu na kuzitupa sakafuni. Zilikuwa zinatoa cheche na kulikuwa na ndimi chache za moto."
Haki miliki ya picha Australian Transport Safety Bureau
Wahudumu walikimbia na kumsaidia kuzima moto huo kwa kumwagilia hedifoni hizo maji kwa kutumia ndoo.
Kufikia wakati huo, betri ya hedifoni hizo pamoja na kifuniko chake cha plastiki vilikuwa vimeyeyuka na kukwamilia sakafuni.
"Kwa sehemu iliyosalia ya safari, abiria walilazimika kuvumilia harufu kali ya plastiki zilizokuwa zimeyeyuka, vipande vya hedifoni hiyo zilivyokuwa vimeungua na nywele za mwanamke huyo ambazo zilichomeka pia," ATSB walisema kupitia ripoti baadaye.
Ripoti hiyo haikusema hedifoni hizo zilikuwa za muundo gani lakini inaaminika kwamba huenda mlipuko huo ulisababishwa na kasoro kwenye betri za lithium-ion zinazotumiwa katika hedifoni hizo.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Simu za Galaxy Note 7 zilikuwa zinashika moto mwaka 2016
ATSB imechangisha mwongozo kuhusu betri na vifaa vingine vinavyotumia betri.
Kumetokea visa kadha vya vifaa vyenye betri za lithium kulipuka na kushika moto kwenye ndege miaka ya hivi karibuni.
Mwaka uliopita, ndege iliyokuwa inajiandaa kupaa kutoka Sydney iliahirisha safari yake kwa muda baada ya moshi kuonekana ukifuka kutoka kwa mkoba uliokuwa umebebwa na abiria.
Baada ya kukaguliwa, ilibainika kwamba kulikuwa na betri ya lithium iliyokuwa imeshika moto.
Mwaka uliopita pia, kasoro kwenye betri zilitambuliwa kuwa chanzo cha simu nyingi aina ya Samsung Note 7 kulipuka na kushika moto.
Samsung ilisitisha utengenezaji na uuzaji wa simu hizo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger