Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yamewakutanisha wahariri ambao ni wanachama
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ili kujadili namna ya kufanya kazi
pamoja na mashirika hayo. Mashirika ya umoja wa mataifa yaliyoshiriki
kwenye mkutano huo ni UNDP, ILO, FAO, WFP, UNHCR, UN Women, nk.
Akizungumza
na wahariri Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez amesema umoja wa
mataifa uko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kuonesha mchango
wao kwenye jamii. Hivyo mchango wa waandishi wa habari ni wa msingi kwao
na ili kuweza kutekeleza malengo waliyojiwekea hasa kuinua uchumi wa
Tanzania.
Mwakilishi
wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini
Tanzania, Alvaro Rodriguez akifungua mafunzo kwa wanachama wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF) ulioandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar
es Salaaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)
Nchini Tanzania Michael Dunford akizungumza jambo kwenye mkutano
uliowakutanisha wahariri wa vyombo kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF) uliowakutanisha ili kujadili njia nzuri za kufanya kazi kwa pamoja
ili kufikisha ujumbe kwenye jamii.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia. Wakimbizi (UNHCR),
Chansa Kapaya akizungumza jinsi wanavyoshirikiana na serikali ya
Tanzania pindi wanapoingia wakimbizi kutoka nchi mbalimbali
zinazoizunguka nchini ya Tanznaia hasa zile nchi zenye migogogro ya
kisiasa.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNAIDS
Dk.Warren Namara akizungumza jambo pamoja natoa data kuhusu maambukizi
ya virusi vya Ukimwi nchini pamoja na duniani na jinsi kiwango hicho
kinavyopunguza nguvu kazi ya taifa.
Katibu
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena akiwasilisha mada
kuhusu mazingira wanayofanyia kazi pamoja na kutolea ufafanuzi kuhusu
jukwa la wahariri Tanzania linavofanya kazi hasa kwenye habari za jamii
kwenye mkutano wao pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa uliofanyika
kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viongozi
mbalimbali wa Mashirika ya umoja wa mataifa nchini Tanzania
wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena kwenye mkutano uliofanyika jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa nchini
Tanzania wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha na wahariri mbalimbali wa
habari kujadili namna ya kufanya kzi ili kufikisha ujumbe kwenye jamii.
Baadhi ya wahariri wakiwa kwenye mkutano huo
Mwakilishi
wa Shirika la umoja wa mataifa la wafanyakazi Duniani (ILO) kwa nchi za
Afrika Mashariki, Mary Kawar akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Baadhi ua Wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza maswali wa wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa nchini Tanzania
Mwakilishi
wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini
Tanzania, Alvaro Rodriguez akijibu maswali yaliyoulizwa na wahariri
kwenye mkutano
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia. Wakimbizi (UNHCR),
Chansa Kapaya akijibu maswali yaliyoulizwa na wahariri.
Mwakilishi
wa Shirika la UN Women Tanzania Bi. Maria Karandenizli akitolea
ufafanuzi swali lililoulizwa na mmoja wa wahariri wakuu kwenye mkutano
uliowakutanisha kujadili namna ya kufanya kazi pamoja na kuwaongezea
uwezo wahariri kwenye utendaji kazi wao wa kila siku.
Mkuu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Nchini Hoyce Temu, akitolea
ufafanuzi baadi ya mambo kwenye mkutano uliowakutanisha wahariri wa
vyombo vya habari mbalimbali kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
ulioandaliwa na mashirika ya umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakichangia mada kwenye mkutano huo
Msaidizi
wa Mwakilishi wa Shirika la Idadi ya Watu UNFPA, Christine Mwanukuzi
akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo kwa wahariri wa habari
yaliyoandaliwa na mashirika ya Umoja wa mataifa yaliyofanyika jijini Dar
es Salaam
Picha
ya pamoja kati ya wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania pamoja na baadhi ya wahariri waliofika kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja kati ya wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania pamoja na wafanyakazi wa mashirika hayo.
SHARE
No comments:
Post a Comment