Moussa Faki Mahamat amechukua rasmi wadhifa wa Rais wa Halmashauri
kuu ya Umoja wa Afrika, huku akiahidi kuifanyia mabadiliko taasisi hiyo
pamoja na kupambana na migogoro mingi inayolikabili bara la Afrika.
Mwanadiplomasia huyo mwenye uzowefu mkubwa, aliwahi pia kuwa waziri mkuu
wa zamani wa Chad. Mahamat mwenye umri wa miaka 56 anaonekana kama mtu
aliyeiwezesha Chad kuteuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kama mwanachama asiye wa kudumu. Mahamat aliteuliwa mwezi Januari
kufuatia duru saba za uchaguzi na kumshinda Waziri wa Mambo ya Nje wa
Kenya, Amina Mohamed, pamoja na wagombea wengine kutoka Senegal,
Botswana and Guinea ya Ikweta. Mahamat, amechukua nafasi ilioachwa na
Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika Kusini aliyepigania mpango wa maendeleo
wa ajenda ya 2063 lakini alionekana kuwa dhaifu katika masuala ya amani
na usalama na alivutiwa zaidi na siasa za nchini mwake Afrika Kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment