Maharamia wa Kisomali wameiteka meli ya kubebea mafuta inayopeperusha
bendera ya Sri-Lanka, hiyo ikiwa mara ya kwanza kwa maharamia hao
kuweza kuiteka meli ya kibiashara tangu mwaka 2012. Afisa wa taasisi ya
kuzuia uharamia John Steed amesema meli hiyo iitwayo Aris 13 ilituma
wito wa msaada jana Jumatatu, na kisha mfumo wake wa kutambulisha mahala
ilipo ulizimwa, na ikabadilisha mkondo wa safari na kuelekezwa katika
bandari ya Alula nchini Somalia. Inaaminika kuwa meli hiyo ilikuwa na
mabaharia wanane. Ndege ya kikosi cha Umoja wa Ulaya cha kupambana na
uharamia Navfor imeruka katika anga ya bahari ilikotekwa meli hiyo
kufuatilia kinachoendelea. Data za shirika la habari la Reuters
zinaonyesha kuwa meli hiyo ilibadilisha njia ghafla, wakati ilipokuwa
ikisafiri kutoka bandari ya Djibouti, kuelekea bandari ya mjini
Mogadishu, Somalia. Wakati wa kilele cha mgogoro wa uharamia mwezi
Januari 2011, kulikamatwa mateka 736 na boti 32.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment